Na Magrethy Katengu, JamhuriMeedia, Dar es salaam

Mamlaka ya Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imewaomba waandishi wa habari za Mtandaoni (digital online) kuhamasisha wananchi kuwa na desturi ya kudai risiti pale wanapofanya manunuzi ili kusaidia kuwapata wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi.

Rai hiyo ameitoa leo Jijini Dae es salaam Mei 29,2024 Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mapato TRA Elimu ya elimu ya mlipa kodi na Mawasiliano kwa Umma Hudson Kamoga katika Semina ya kwanza na Jukwaa la Waandishi wa habari wa Mtandaoni (JUMIKITA) ambapo amesema waandishi hawana budi kuwa wazalendo na taifa lao kuweza kumsaidia Rais kwa kuwaelimisha wananchi kudai risiti pale wanapofanya manunuzi kwani kodi ni fedha inayosaidia miradi mbalimbali ikiwemo Barabara, hospitali,shule.

“Tunatambua kuwa dunia imekuwa kijiji kwa ajili ya Mitandao ya kijamii hivyo kundi hili la waandishi wa habari wa mtandao watatusaidia sanaa kwani kuna wafanyabiashara wengi wanafanyabishara kidigital kupitia semina hii italeta tija kwa Wananchi kukusanya mapato huko walipo na kuwajengea utamaduni wa kulipa kodi kidigitali bila usumbufu wowote” amesema Kamoga

Hata hivyo amesema kuna utaratibu wa kukusanya kodi kwa njia ya mtandao kwani wamegundua kuna baadhi ya wafanyabishara hawana ukaazi Tanzania lakini shughuli zao hutumia hutumia mitandao ya kijamii kukutana na wateja wao hivyo kupitia wanahari wa mitandao watasaidia kuwafikishia elimu ya namna ya kulipa kodi .

Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanaandishi wa habari Mtandaoni JUMIKITA, Shabani Matwebe ameshukuru sana TRA kutambua mchango wa wanahabari wa mtandaoni kwa kuwapatia semina adhimu kwa mara ya kwanza hivyo italeta tija kuongezeka kwa mapato kwani wale wanaotumia simu janja wataipata elimu huko huko walipo.