Add caption

 

Meneja Uhusiano wa TTCL Tanzania, Ndugu Nicodemus Thom Mushi (kulia), akikabidhi msaada wa vyakula na mahitaji mengine kwa niaba ya Mkugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Bw. Waziri Kindamba kwa watoto waishio katika mazingira magumu ili kuwawezesha kufurahia Sikukuu ya Eid. Anayepokea kushoto ni Mamamlezi wa Kituo cha watoto yatima cha Mwana, Saada Omar Ally kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam.

 

Meneja Uhusiano wa TTCL Tanzania, Ndugu Nicodemus Thom Mushi (kulia), akikabidhi msaada wa vyakula na mahitaji mengine kwa niaba ya Mkugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Bw. Waziri Kindamba kwa Sista Makrina Kapinga (kushoto) mlezi wa Kituo cha watoto yatima cha DMI kinachosimamiwa na Shirika la Mabinti Immakulata cha Kibamba, jijini Dar es Salaam.

 

Meneja Uhusiano wa TTCL Tanzania, Ndugu Nicodemus Thom Mushi (kulia), akikabidhi sehemu ya msaada wa vyakula na mahitaji mengine kwa niaba ya Mkugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Bw. Waziri Kindamba kwa Mamamlezi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Mwana, Saada Omar Ally (kushoto) kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam akipokea sehemu ya msaada huo.
SHIRIKA
la Mawasiliano Tanzania TTCL Corporation, limetoa msaada wa vyakula na mahitaji
muhimu kwa watoto waishio katika mazingira magumu ili kuwawezesha kufurahia Sikukuu
ya Eid.
 
Msaada huo umetolewa kwa
Vituo vya DMI kilichopo Kibamba Kibwegere chenye watoto 60 na Kituo cha Mwana kilichopo
Vingunguti chenye watoto 85 vyote vikiwa jijini Dar es Salaam.
 
Akikabidhi misaada hiyo
kwa niaba ya Mkugenzi Mkuu wa TTCL Corporation Bw. Waziri Kindamba, Meneja Uhusiano
wa TTCL Tanzania, Ndugu Nicodemus Thom Mushi amesema,
Shirika lake linatekeleza kikamilifu wajibu wa Taasisi za Umma na Binafsi wa kutoa
sehemu ya mapato yake kwa ajili ya ustawi wa Jamii na kuleta unafuu kwa maisha ya
watu wanao wazunguka.
 
“Huu ni utaratibu wetu
wa kila mara hali inaporuhusu, tunajitoa kwa ajili ya wahitaji na hasa watoto wa
naoishi katika mazingira magumu ili kuwapa matumaini ya kujiendeleza ki-elimu na
kujitegemea ili kuwa raia wema wasiku za baadae. Tuna waomba Watanzania watuunge
mkono kwa kutumia huduma zetu ili kutupa nguvu ya kuendelea kusaidia jamii kwa matendo
mema kama haya,” alisema Ndugu Thom Mushi.
 

 

Wakishukuru kwa misaada
hiyo, Viongozi wa vituo vyote viwili wameiomba TTCL na Taasisi nyingine kuendelea
kusaidia makundi ya watu wenye mahitaji maalumu na hasa watoto wenye ndoto nyingi
za kubadili hali zao za maisha na kuchangia maendeleo ya Taifa.
Meneja Uhusiano wa TTCL Tanzania, Ndugu Nicodemus Thom Mushi (kulia), akikabidhi sehemu ya msaada mmoja wa watoto (kushoto) wa kituo cha DMI inachosimamiwa na Shirika la Mabinti Immakulata cha Kibamba, jijini Dar es Salaam.

 

Meneja Uhusiano wa TTCL Tanzania, Ndugu Nicodemus Thom Mushi pichani akifurahi na watoto wa kituo cha DMI mara baada ya kukabidhi msaada wa vyakula na mahitaji mengine kwa niaba ya Mkugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Bw. Waziri Kindamba kwenye kituo hicho.

 

Baadhi ya maofisa wa TTCL Tanzania waliotembelea Kituo cha Yatima cha DMI kinachosimamiwa na Shirika la Mabinti Immakulata (masista) cha Kibamba, jijini Dar es Salaam wakifurahi kwa pamoja na watoto wa kituo hicho mara baada ya kukabidhi msaada huo kwa watoto.

 

Watoto wanaolelewa katika Kituo cha Yatima cha DMI kinachosimamiwa na Shirika la Mabinti Immakulata (masista) cha Kibamba, jijini Dar es Salaam wakiwakaribisha baadhi ya maofisa wa TTCL Tanzania kwa nyimbo walipowatembelea na kutoa msaada.
Please follow and like us:
Pin Share