Na Isri Mohamed

Bondia Mtanzania Twaha Kiduku Amefanikiwa Kumchakaza Mpinzani wake kutoka India, Harpreet Singh kwa ‘TKO’ raundi ya tano.

Ushindi huo wa Kiduku umepatikana baada ya Singh kumuomba refa amalize pambano bila kuelezea nini hasa kimemkuta.

Baada ya kumaliza pambano Hilo ambalo si la ubingwa, Kiduku amesema ilikuwa kiu yake kupata ushindi kwa ‘KO’ kwani mashabiki zake wamekuwa wakilalamikia kutorudhishwa na kiwango chake katika mapambano yake kadhaa yaliyopita.

Pambano Hilo Limechezwa usiku wa Kuamkia Leo katika ukumbi wa Tanzanite Hall, mkoani Morogoro.

By Jamhuri