UFAFANUZI WA KUKAMATWA KWA GARI YA MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM

Ndugu waandishi wa habari. Napenda kutumia fursa hii kuwapa pole wananchi wa jiji la Dar es Salaam kutokana na taarifa ambazo zimeripotiwa leo kwenye baadhi ya magazeti.

Jumamosi ya Tarehe 27 Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita alishiriri kwenye kampeni za mgombea  Ubunge wa Jimbo la Kinondoni Salum Mwalimu ambapo. Ambapo kabla ya kufika kwenye eneo mbalo kampezni hizo zinafanyika Dereva alimshusha  Meya ,na kuchukua gari nyingine kuelekea kwenye eneo ambalo kampeni hizo zilikuwa zikifanyika.

Kwakuwa Magari ya serikali hupaki kwenye Taasisi za Umma,  Dereva alikwenda kupaki gari kwenye ofisi za Chama Cha Mapinduzi CCM. Hata hivyo baada ya muda , walijitokeza vijana kadhaa na kutoa upepo gari hiyo bila kufahamu sababu  wakati huo ambapo dereva na wenzake  wawili walikuwa wameenda kula.

Ndugu  waandishi wa habari. Baada ya kufanyika kwa tukio hiko, licha ya dereva huyo kujieleza na kutoa vitambulisho kuwa ni mtumishi wa serikali nasio wa chama, bado waliendelea kumtuhumu kwamba alikuwa na lengo la kuvuruga uchaguzi na hivyo walimkamata, wakampiga na baade alipelekwa kituo cha polisi Magomeni kwa ajili ya kuhojiwa.

Naomba ifahamike kuwa Meya wa jiji hawezi kujihusisha kwenye matukio ya kupanga njama  zozote kwa ajili ya kufanya vurugu kwenye matukio yoyote ya kisiasa hususani kwenye uchaguzi.

Ndugu waandishi wa habari. Napenda kuwaeleza wananchi wa jiji la Dar es Salaam kuwa, Meya wa jiji hakuwahi kushiriki,wala kujihusisha na matukio yoyote ya kufanya vurugu wakati wakampeni za uchaguzi wala matukio ya kisiasa kama ambavyo taarifa hiyo imetolewa na Vijana wa UVCCM.

Mazungumzo ambayo yalikuwa yakifanyika kwa kutumia ujumbe mfupi wa maandishi kwa njia ya simu ,ilikuwa ni baina ya Dereva na Katibu wa Meya ambapo alikuwa akipewa taarifa kuhusu kukamatwa kwa gari hiyo. Ambapo namba hizo ni 0784………16 dereva, katibu ni 0717 …….52.

Meya wa jiji amewahi kushiriki kampeni za uchaguzi mdogo wa marudio ya Udiwani kata ya Kijichi lakini haikuwahi kutokea vurugu yoyote. Hivyo taarifa ya kusema kwamba amekuwa akijihusisha kwenye matukio hayo hazina ukweli wowote na kwamba zinalenga kulichafua jina na heshima kubwa ya kisiasa aliyojiwekea tangu achaguliwe kuliongoza jiji hili.

Meya wa jiji amekuwa akifanya kazi zake za kuliongoza jiji bila kuwepo na mvutano na kiongozi yoyote serikalini, kisiasa, licha ya kwamba nafasi yake inatokana na chama cha upinzani. Lakini  ielewe kuwa kushiriki kwakwe kwenye kampeni hakukuwa na maana ya kupanga njama yoyote ya kihalifu bali alihudhuria kama viongozi wengine wanavyo hudhuria kwenye shuguli hizo.

Meya wa jiji amesikitishwa na kulaani vikali kitendo cha kukamatwa kwa gari lake na kutolewa upepo Dereva wake hali ya kuwa ni mtumishi wa serikali na kwamba jambo hilo linapoteza taswira bora ya katika uongozi.

Gari ya serikali kupaki kwenye ofisi yoyote sio jambo baya kwa kuwa haikuwa na bendera ya chama na kwamba hakukuwa na sababu za kulikamata na kuihuisha kwa mbinu mbaya ambayo inalenga kuchafua sifa ya jiji.

Hivyo niombe jeshi la polisi kwakuwa wote ni watumishi wa serikali, wanawatumikia wananchi, kama itawapendeza kufanya uchunguzi wao wa kina kuhusiana na jambo hili, ikiwa ni pamoja na kutenda haki bila kujali kwamba tukio hili linatokana na mtu wa chama gani.

Imetolewa leo Januari 29, 2018 na

Christina Mwagala, Ofisa habari na Msemaji Mkuu wa Mshiki Meya wa jiji la Dar es Salaam.