Ujamaa hauna uhusiano na ragi, wala nchi atokayo mtu. Mtu
yeyote mwenye akili, mwenye kuamini Ujamaa au asiyeamini, anafahamu
kwambawako waminio Ujamaa katika nchi za Kibepari, na wanaweza
kupatikana waaminio Ujamaa kutoka nchi za Kibepari. Mara nyingi watu
wa namna hiyo wanakuja kufanya kazi katika nchi changa zilizo na siasa
ya Ujamaa kama Tanzania, kwa sababu wanakerekwa na ubepari wa
kwao. Wala mtu mwenye akili hafumbi macho akasahau kwamba kuna
mabepari wanaokereka katika nchi za Ujamaa_ kama vile vile ambavyo
wataonekan mabepari wanaokereka katika Tanzania.inawezeakana hata
ukapata baadhi ya wale mabepari wanaomia katika nchi za
masharikiwakaja kufanya kazi kwetu.
Wala haifai mtu mwenye kuamini Ujamaa kuwadhania mabepari
wote kama mashetani. Kuuchukua ubepari ni jambo moja, na kujaribu
kuwauzia watu wasiwe na matumaini ya ubepari ni jambo jingine kabisa.
Lakini itakuwa upumbavu kwetu kuudhania mabepari wote kuwa
wanamapembe, kama vile vile ilivyo ujinga kwa watu wa ulayakudhania
kuwa sisi Watanzania sasa tumekuwa vibwengo.
Kwa kweli viongozi wan nchi za kibepari sasa wameanza
kutambua kwamba makoministi ni binadamu kama wao, na makomunisti
si vibwengo. Na siku moja watatambua pia kwamba hata makomunisti wa
Kichina watu pia itakuwa ujinga kwetu tunaoucheka upumbavu huo,
amabao wenzetu wanaanza kuutambua na kuerevuka , halafu sisi
wenyewe tuzame katika upumbavu huo huo kwa kuto kuwathamini
binadamu wa aina nyingine laizma, katika maneno na matendo yetu,
tutambue kuwa mabepari ni binadamu kama vile vile wapend aUjamaa
walivyo. Wanaweza kuwa wanakosea; na kwa kweli ndivyo tusemavyo
sisi tunaopenda Ujamaa. Lakini kaiz yetu ni kuuziba ubepari usitawale.
Kazi yetu sis sio kuwatesa mabeoari, au kuwafanya wale wanaotumaini
ubepari washindwe kuishi kwa raha na heshima.
Kusema kweli ni lazima wapenda Ujamaa wafikirie matatizo hayo,
wafikirie jinsi vyombo vyetu vinavyioweza watu katika nchi yetu.
Kujaribu kuwabagua watu wanaofanya kazi kwa faida ya taifa letu,
wengine wakawa ‘wema’, na wengine ‘wabaya’, kwa sababu tu ya rangi
ya ngozi yao, au nchi wanayotoka, au asili ya kabila lao, ni kuharibu kazi
tuliyo ianza. Yafaa tutazame kama mtu anaiweza kazi yake kwa manufaa

ya nchi. Ila, wale baadhi yetu tunaojidai kuwa watalaamu wa maisha ya
binadamu, lazima pia tuwe na mawazo ya kitaalamu na yasipoendelea
wakati tunafanya uamuzi huo. Lazima tufikirie watu kwa ujumla, au mtu
binafsi, siyo ‘Mwasia’, au’Mzungu’, au ‘Marekani’, na kadhalika.
Jambo la hakika ni kwamba Ujamaa katika Tanzania utajengwa na
Watanzania. Na tunafanya juhudi tufikie wakati ambapo watu wote
watakao fanya kazikatika serikali yetu watakuwa Watanzania weusi.
Lakini itakuwa ujinga kwa mtu yeyote kudhani kwamba , kwa sabau tuna
watu wasio Watanzania wanaofanya kazi serikalini na katika makampuni
yaliyo chukuliwa na serkali, basi sisi hatuendeshi mambo yetu yenyewe .
wanaoeweza kusema hivyo kwa wakati huu ni wale tu ambao hawajiamini
wenyewe, au wale ambao wnajaribu kuficha udhaifu wao. Maana una
ushahidi wote unaonyesha kinyume cha mawazo hayo. Tulipata uhru
wetu, ingawa tulikuwa tunatawaliwa na wakoloni. Tukawa Jamuhuri
ingawa tulikuwa tunatawaliwa na wageni wengi waliokuwa wakifanya
kazi hapa, na wakati,wakishika madaraka makubwa. Tuliukamilisha
mwungano wa Tanganyika na Zanzibar, ingawa watumishi wengi wa
Tanzania bara walikuwa wametoka katika ambazo hazikupenda mapinduzi
ya Zanzibar. Tumelikubali Azimio la Arusha, na mnamo wiki moja
tumechukua au kuyatwala makampuni yote makubwa ambayo yanaweza
kuutawala uchumi wetu. Na katika mambo yote hayo tumetumia
wafanyakazi wa Serkali wo wote waliohusika . na wote , walio
Watanzania na wasio Watanzania , wanatimiza maagizo yetu kwa
uaminifu, na wanafanya kazi kwa bidii sana.
Azinio la Arusha linlozungumza habari za binadamu, na imani zao.
Linazungumza habari za ubepari na ujamaa, na habari za wapenda ujamaa
na mabepari. Halizungumzii habari za rangi au umataifa. Kinyume chake,
Azimio linasema kwa wote wanaosimamia haki za wakulima na wafanya
kazi mahali popote ulimwenguni ni rafiki zetu. Ndiyo kusema kwamba
yatupasa kufikira tabia na uwezo wa kila mtu; tusiwatmbukize watu katika
mafungu yaliyokwisha pangwana rangi au taifa, halafu tunawahukumu
kuwa wema au wabaya. Na hakika mtu hawezi kusema anapenda Ujamaa
bila ya kujaribu kutenda matendo ya Kijamaa. Maana ikiwa tunataka
vitendo vilivyofnaywa kutokana na Azimio la Arusha view na maana kwa
watu, basi lazima tukubali msingi wa umoja wa binadamu. Jambo kubwa
sasa ni kufanikiwa kwa kazi hii tuliyoianza. Rangi, au anakotoka mtu
anaefanya kazi kufikia lengo hilo haidhuru hata kidogo. Na kila mmoja
wetu lazima ashindane na nafsi yake kuondoa mawazo na desturi za
ubaguzi amabzo ni sehemu ya mambo tuliyoyarithi kutoka Ukoloni.

Si jambo rahisi kuzigeuza tabia kama hizo. Lakini siku zote
tumetambua kuwa ni jambo la lazima, na kwamba unagzi ni kitu kibaya.
Tulipigania uhuru kwa msingi huo. Usawa wa binadamu ndiyo neo la
kwanza katika imani za TANU inaamini {a} kwamba binadamu wote ni
sawa, {b} kwamba kila mtu nastahioli heshima.
Ili tufanikiwe kuujenga Ujamaa katika nchi hii lazima kila
mwananchi , na hasa kila uongozi wa TANU, lazima aishi kwa imani
hiyo. Na tukumbuke vitu viwili. Kwanza, tumeamua kujenga Ujamaa
katika Tanzania. Na pili, Ujamaa na Ubaguzi haviendi pamoja.
Elimu ya kujitegemea
Tangu siku nyingi kabla ya uhuru watu wan chi hii, chini ya
uongozi wa TANU, wamekuwa wakidai elimu zaidi kwa watoto wao.
Lakini bado hatujakaa na kufikiri kwanini tunakaa na kutaka elimu: ina
shabaha gani. Kwahiyo, inagawaje kwa siku nyigni mafunzo
yanayotolewa katika katika shule yametolewa kimakosa, lakini mpaka
sasa hatujaitoa makosa misingi yenyewe ya elimu tuliyoirithi wakati
tulipopata uhru wetu. Hatujafanya kwa sababu kwa kweli hatujafikiria
badio habari ya mipango ya elimu, isipokuiwa katika kupata walimu,
mainjinia, mabwana shauri,n.k.kila mtu binafsi, na hata sotekwa pamoja
tumefikiria elimu kama mafunzo ya kazi ya kujipatia mishahara mikubwa
katika kazi za siasa.

Please follow and like us:
Pin Share