Waziri mkuu wa Ukraine ameiambia BBC kutakuwa na “Vita vya Tatu vya Dunia” ikiwa Ukraine itashindwa katika mzozo kati yake na Urusi, huku akilitaka bunge la Marekani kupitisha mswada wa msaada wa kigeni uliokwama kwa muda mrefu.

Denys Shmyhal alionyesha “matumaini makubwa” kwamba wabunge wa Marekani wangepitisha mswada huo unaokumbwa na mvutano mkali, ambayo inajumuisha dola bilioni 61 zilizotengwa kwa ajili ya Kyiv.

Baraza la Wawakilishi linatazamiwa kupigia kura kifurushi hicho Jumamosi hii. Pendekezo hilo linajumuisha ufadhili kwa Israel pamoja na maeneo ya bahari ya Hindi na Pacific.

Akizungumza na BBC mjini Washington DC siku ya Jumatano, Waziri Mkuu Shmyhal alisema kuhusu usaidizi wa usalama wa Marekani: “Tunahitaji pesa haraka iwezekanavyo.” “Kama hatutalinda… Ukraine itaanguka,” aliongeza.

“Kwa hivyo mfumo wa usalama wa kimataifa utaharibiwa … na ulimwengu wote utahitaji kupata … mfumo mpya wa usalama. “Au, kutakuwa na migogoro mingi, aina nyingi za vita, na mwisho wa siku, inaweza kusababisha Vita vya Tatu vya Dunia.”

Hii si mara ya kwanza kwa Ukraine kutoa onyo hilo la kutisha kuhusu matokeo ya uwezekano wa kushindwa kwake.

Please follow and like us:
Pin Share