Na Magrethy Katengu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Serikali kupitia Wizara ya Afya katika Kipindi cha mwaka 2023 imejitahidi kwa kusogeza huduma kwa wananchi kwani asilimia 60 ya wananchi wanapata huduma ndani ya kilometa 5 hivyo mwaka 2023 vituo vya afya ni 9366 kutoka vituo 8881 2022 ni ongezeko la vituo 485 sawa na asilimia 5.5

Taarifa hiyo ya hali ya utoaji huduma ya afya mwaka 2022, 2023 imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri Afya Ummy Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema vituo hivyo ni vingi na Zahanati zinabeba asilimia 83 ya vituo vyote vya kutolea huduma za afya na vituo viko asilimia 12 hali hiyo inaonyesha Watanzania wengi wanatibiwa katika Zahanati na Vituo vya afya.

Waziri Ummy amebainisha kuwa katika mwaka huo 2023 idadi ya vitanda vya kulaza wagonjwa imeongezeka hadi kufikia vitanda laki moja ishirini na sita elfu miambili na tisa ambapo mwaka 2022 ilikuwa vitanda laki moja na nne mia sita themanini na saba ambapo vigezo vilivyowekwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), limeweka viwango vyake katika kila watu 1000 kuwe na vitanda vya kulaza wagonjwa 2.5 naTanzania bara vitanda vilivyopo ikigawanywa na idadi ya Watanzania ni sawa na vitanda 12.1 katika kila watu 1000 hivyo karibia inakaribia vigezo vya WHO.

“Idadi ya vitanda kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa mahutihuti katika vituo vya serikali Desemba 2022 vilikuwa vitanda 528 huku Desemba 2023 vimefikia 1000 ongezeko hili inasaidia kupunguza vifo vinavyotokea hospitali ambavyo vinaweza kuzuilika kwa asilimia 20 hadi 30” amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy akizungumzia pia huduma za uchunguzi wa magonjwa ikiwemo misuli , mishipa ya damu na fahamu, ubongo na uvimbe Mashine za MRI Desemba 2022 zilikuwa 6 huku Desemba 2023 zimeongezeka na kufikia 13 pia Mashine ya Sit scan zinazotumika kuchunguza misuli ubongo na viungo vya mwili Desemba 2022 zilikuwa 22 huku Desemba 2023 zimeongezeka na kufikia 45 na zimeanza kufanya kazi katika mikoa isipokuwa Mara,Songwe, Kigoma, Katavi,Rukwa zimefika ila bado hazijaanza kutumiwa.

Hata hivyo amebainiasha kuwa Ugonjwa wa sukari, shinikizo la juu la damu, mfumo wa hewa, UTI na ugonjwa kuharisha ni miongoni mwa magonjwa 10 yaliyosumbua wananchi wengi nchini kwa mwaka 2023.

Ummy Mwalimu amebainisha takribani watu watu 6,52,455 sawa na asilimia 2.5 yaligundulika kuwa na ugonjwa wa sukari katika mwaka 2023.

“Zamani miaka kama mitatu nyuma tulikuwa hatuoni kisukari wala shinikizo la juu la damu katika magonjwa 10 yaliyokuwa yakiongoza katika wagonjwa wa nje nchini, tutaeleza ni lipi ambalo tumejipanga kufanya,”amesema Ummy

Amesema, kwa upande wa watoto chini ya umri wa miaka mitano maambukizi ya mafua na kikohozi ni asilimia 38.8.

“Kwa hiyo katika kila watoto 100 mwaka 2023 waliokwenda kwenye Vituo vya kutoa huduma za afya watoto takribani 39 walikwenda kwa sababu au waligundulika maambukizi katika mfumo wa hewa wa juu, malaria nayo imekuja juu kwa asilimia 10.7.” amesema Ummy na kuongeza

“Ugonjwa wa kuharisha bila upungufu wa maji ni asilimia 8.4, maambukizi kwa njia ya mkojo asilimia 7.5, Homa ya Mapafu/Nimonia asilimia 7.4, maambukizi ya ngozi asilimia 3.8, magonjwa mengineyo ya mfumo wa chakula, magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza asilimia 3.8

Katika hatua nyingine uchunguzi umebaini kuwa 2022 watu 163, 131 wamegundulika kuwa na maambukizi mapaya ya virusi vya ukimwi (VVU) kwa mwaka 2023.

Amesema, jumla ya watu 8,145,576 walipima Virusi vya UKIMWI (VVU) na Watu 163,131 kati yao walingundulika kuwa na maambukizi ya

Ugonjwa wa UKIMWI, Serikali iliendelea kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI ambapo katika mwaka 2023 jumla ya Watu 8,145,576 walipima Virusi vya UKIMWI (VVU) kulinganisha na Watu 6,930,758 mwaka 2022 (DHIS2 2023),”amesema na kuongeza;

“Kati ya watu waliopima mwaka 2023, watu 163,131 waligundulika kuwa na maambukizi ya VVU ukilinganisha na watu 182,095 mwaka 2022 (DHIS2 2023),”amesema.

Aidha, amesema waliokuwa wanatumia dawa za kufubaza virusi vya VVU walikuwa 1,663,651 kulinganisha na watu 1,612,512 (DHIS2023)

“Mwaka 2023, vifo vitokanavyo na UKIMWI vilikuwa 22,000 kulinganisha na vifo 29,000 mwaka 2022(Spectrum 2022),”amesema Ummy.

By Jamhuri