Ummy: Tanzania bado ina uhaba wa madaktari bingwa

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema Tanzania bado ina uhaba mkubwa wa Madaktari Bingwa hivyo uwepo wa mpango wa kambi ya upasuaji wa huduma za kibingwa unahitajika sio kwa mkoa wa Tanga bali ni mikoa yote nchini.

Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM), ameyasema hayo wakati akizindua mpango wa kutoa huduma za upasuaji wa kibingwa bila malipo kwa wakazi wa Jiji la Tanga uliofanyika kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo.

Amesema hivyo uwepo wa mpango huo utawasaidia wana Tanga na watanzania kwa ujumla kupata matibabu, dawa, vifaa tiba bila gharamu yoyote.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa uzinduzi wa  mpango wa kutoa huduma za upasuaji wa kibingwa bila malipo kwa wakazi wa Jiji la Tanga

Mpango huo ambao utasaidia kufanya upasuaji utafanywa na madaktari bingwa kutoka Taasisi ya Peleks Humanitarian Organizationya nchini Uingereza ambapo jumla ya wagonjwa 380 watafaidika kati yao wagonjwa zaidi ya 700 waliofanyiwa uchunguzi.

Kambi hiyo ya matibabu Bingwa ya upasuaji imewezeshwa na Taasisi ya Watumishi Health Check, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Tanga mjini ambap kwa pamoja wamewaleta wataalamu hao wa upasuaji kutoka nchini Uingereza.

Awali akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi wa Watumishi Afa Check Dkt Siraji Mtulia alisema kuwa upasuaji huo utafanyika kuanzia Novemba 5 hadi 11 mwaka huu na utagharimu milioni 876.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt Seif Kallage akizungumza wakati wa halfa hiyo

Naye kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt Seif Kallage amesema uwepo wa kambi hiyo ni jitihada za Waziri Ummy kwa sababu ni jukumu ambalo amepewa na Rais Samia Suluhu kuhakikisha afya za watanzania vinaimarika na kuboresha huduma.

Amesema hata ukiangalia ile kampeni ya Mama Samia yeye ndio anaiendeleza amenza na Tanga kwa kushirikiana na Peleck anataendelea na mikoa mengine nchini.

Hata hivyo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Jonathan Budemu alisema kwamba kambi hiyo itaweza kuwasaidia wananchi na katika watu 700 walionwa na madaktari walikuwa hawana uharaka ule na muendelezo wa kambi hii utawasaidia kuweza kuwaonaa.

Baadhi ya madaktari bingwa wakiwa kwenye uzinduzi

Alisema katika kambi hiyo watakuwa na changamoto ya vitanda hivyo Mstahiki Meya wale ambao watakosa maeneo ya kuwaweka wanaomba kuwaweka kwenye vituo vyengine baada ya upasuaji kama Ngamiani na Makorora na vya jirani ili wote waweze kupata huduma kwa wakati.