Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Festo Dugange amesema kuwa Serikali imeweka mpango mkakati wa ukamilishaji wa ujenzi wa vituo vya afya vyote nchini kwa lengo la vituo hivyo kuanza kutoa huduma kwa jamii.

Ameyasema hayo leo Novemba, 3, 2022 Bungeni, Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Nyongeza la Mbunge wa Igalula Venant Daud Protus aliyetaka kujua ni lini Serikali itapeleka fedha ya kumalizia vituo vya afya ili wananchi waendelee kupata huduma za afya nchini.

Halimashauli zatakiwa kuainisha maeneo ujenzi wa vituo vya Afya.

Mhe.Dugange amesema kuwa Serikali imekuwa ikijenga vituo vya afya kwa awamu, ambapo kwa awamu ya kwanza kiasi cha shilingi milioni 250 kilipelekwa kwa ajili ya ujenzi wa vituo na fedha kwa ajili ya ukamilishaji zilipelekwa kiasi cha shilingi milioni 250.

Amesema kuwa Serikali imefanya tathmini ya vituo vya afya ambavyo ujenzi wake ulianza na haujakamilika na inampango wa kuhakikisha vituo hivyo vinakamilika ili kuendelea kutoa huduma kwa jamii.

Akijibu swali la msingi la mbunge viti maalumu Jaqueline Andrew Kainja aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuongeza majengo katika Kituo cha Afya Itobo Wilayani Nzega, Dugange amesema Serikali imeshaanza kuongeza majengo katika kituo cha afya Itobo kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Nzega na imetoa shiling million 500 kwaajili ya ujenzi wa jengo la kuhudumia wagonjwa wa nje, jengo la maabara, kichomea taka, jengo la mama na mtoto, jengo la upasuaji, na jengo la kufulia nguo.

By Jamhuri