Rais wa Urusi Volodymyr Zelensky amesema Urusi imefanya mashambulizi makali ya usiku kucha kwa kutumia zaidi ya makombora 90 na droni 60 aina ya Shahed zilizotengenezwa na Iran.

Rais wa Urusi Volodymyr Zelensky amesema leo kuwa Urusi imefanya mashambulizi makali ya usiku kucha nchi humo kwa kutumia zaidi ya makombora 90 na droni 60 aina ya Shahed zilizotengenezwa na Iran katika moja ya mashambulizi makubwa zaidi ya hivi karibuni.

Rais huyo amesema kuwa ulimwengu unaona shabaha za magaidi wa Urusi kwa uwazi mno ambazo zinajumuisha viwanda vya nishati, bwawa la umeme unaotengenezwa kutokana na maji na hata majengo ya kawaida ya makazi.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ukraine imesema kuwa mashambulizi hayo yamesababisha vifo vya watu wawili na kujeruhiwa kwa wengine 14 wakati watu wengine watatu hawajulikani walipo.

Wizara hiyo imeendelea kusema kuwa huduma zao zote sasa zinahusika katika kukabiliana na athari za shambulizi hilo na kwamba wanatumia vifaa vya roboti katika maeneo hatari kupunguza majeraha kwa wakokoaji.

Kwa mara nyingine tena, Zelensky ametoa wito wa msaada wa silaha kutoka kwa mataifa ya Magharibi.

By Jamhuri