Wakati mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akitangaza maandalizi ya kufuru ya bethidei ya mwanaye Tiffah (pichani), utata umeibuka baada ya upande wa pili wa mzazi mwenziye msanii huyo, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kudaiwa kuipotezea.

Mtu wa karibu na familia ya Diamond ameeleza kuwa, Zari hajakubaliana na ‘mbwembwe’ zinazoandaliwa na msanii huyo kwa ajili ya shughuli hiyo hivyo ameamua kukaa kimya.“Yaani unaambiwa mama la mama (Zari) kafura, kaamua kuichunia baada ya kupishana na Mond katika suala zima la maandalizi ya bethidei hiyo.

“Inaonekana kuna kitu hususan katika mambo yao ya kibiashara maana si unajua wale kwao kila kitu ni biashara sasa linapokuja suala la bethidei kuna makampuni ambayo yanajitokeza sasa mamaa asipokubaliana na kitu ndo’ maana unaona hivi,” alinyetisha mtu huyo. Kudhihirisha kwamba Zari ameipotezea bethidei hiyo hususan inayoandaliwa na Diamond, chanzo hicho kilieleza kuwa, mrembo huyo wa Kiganda mwenye maskani yake pande za Sauz amekuwa kimya na hasapoti chochote kinachowekwa na Diamond.

“Wewe ingia Insta (mtandao wa Instagram) utaona tu, Zari hasapoti chochote tangu Diamond ameanza mbwembwe za kuinadi bethidei. Hakomenti wala yeye haposti kuhusu bethidei ya Tiffah. Kama hiyo haitoshi, hata akaunti ya Tiffah yenyewe haiongelei chochote kuhusu bethidei yake,” kilidai chanzo hicho.

Amani liliingia kurasa za Zari na Tiffah katika mtandao wa Instagram na kujiridhisha kwamba akaunti za wawili hao, hazisapoti chochote kinachopostiwa na Diamond kuhusu bethidei hiyo kubwa inayoelezwa kuwa itasherehekewa kwa takriban siku sita mfululizo pande za Sauz.

Amani pia ‘lilifukua makaburi’ kwa kuperuzi bethidei ya mwaka jana ya Tiffah na kukuta, Diamond na Zari walikuwa wakisapotiana kuisherehesha sherehe ya Tiffah ambayo awali ilikuwa ifanyike katika Ukumbi wa Mlimani City lakini ikaahirishwa, ikafanyikia nyumbani.

UTATA MWINGINE

Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, utata mwingine uliogubika bethidei ya Tiffah ni kitendo cha Diamond kutaka kuitelekeza bethidei ya mtoto wake aliyezaa na mwanamitindo Hamisa Mobeto, Dylan jambo ambalo limesababisha minong’ono ya chinichini kutoka kwa Team Mobeto.

“Watu wa Mobeto wameanza kumnanga Diamond na kumwambia haiwezekani amuache Dylan ambaye bethidei yake ni Agosti 8, halafu aende kufanya bethidei ya Tiffah Agosti 17, mwaka huu. “Tutapiga kelele kweli mitandaoni asitufanyie hivi kwani huyu Dylan sio mwanaye? Kwa nini wao wote kuanzia Diamond, Esma na mama yake Diamond wapendelee kule na si huyu wa mtoto wa huku nyumbani?” kilimwaga ubuyu chanzo hicho.

DIAMOND HUYU HAPA

Juzi, Amani lilimvutia waya Diamond akiwa nchini Marekani na kumuuliza juu ya utata ulioibuka ambapo kwa upande wake alisema haoni tatizo kwani wote ni watoto wake na Dylan atawakilishwa na mama yake (Mobeto) pamoja na bibi yake (mama Mobeto). “Mimi sioni tatizo. Nitakwenda Sauz sababu nitakuwa nimemaliza ‘tour’ yangu ya muziki lakini huko nyumbani, Mobeto ni mzazi mwenzangu pia, ataniwakilisha pamoja na mama yake Mobeto,” alisema Diamond.

Please follow and like us:
Pin Share