Na David John,JamhuriMedia

SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Hassan Suluhu imeamua kuwekeza katika vyuo vya ufundi na ikapanua huduma zake katika Chuo cha VETA wilayani Karagwe ambapo awali kulikuwa na vyuo vya mkoa na vyuo ambavyo vilikuwa kwenye kanda.

Akizungumza na waandishi wa habari waliofika chuoni hapo Mkuu wa Chuo cha VETA Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera Pascal Thomas,amesema kuwa,chuo hicho ni miongoni mwa vyuo wilayani humo na kinachotoa huduma bora.

Amesema kuwa wao Karagwe wapo kanda ya ziwa ambayo inaunganisha mikoa ya Mwanza,Mara,Kagera pamoja na Geita na katika Mkoa wa Kagera ambao una Wilaya ya Karagwe, Misenyi,Kyerwa ,Ngara ,Muleba,Biharamuro pamoja na Bukoba hivyo katika vyuo ambavyo vimepandishwa hadhi ni pamoja na chuo cha Karagwe ambapo chuo kihistoria kiliaza mwaka 1986 na kilikuwa kinamilikiwa na mtu binafsi ambaye alikuwa marehemu Edmin MkendaKenda.

Thomas amefafanua kuwa baada ya aliyekuwa mmiliki wa chuo hicho kuona gharama za uendeshaji zinakuwa kubwa ndipo aliamua kukabidhi kwa Halmashauri ya wilaya hiyo tangu mwaka 1992 na kuanzia mwaka huo chini ya Halmashauri ya wilaya kiliendelea kutoa huduma ya mafunzo ya ufundi nchini hivyo mpaka sasa hivi kinaendeshwa na Serikali kwa asilimia mia moja.

“Tunamshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa mna anavyowezesha Chuo cha VETA wilayani Karagwe ,chuo cha Veta karagwe kinauwezo wa kupokea vijana 250 wa kwa kozi ndefu lakini hata kina kozi fupi fupi ambazo zinaendeshwa zaidi ya vijana 450 ambao tunaweza kuwapokea kwa mwaka hivyo uwezo wake hadi hivi sasa ukiweka kozi ndefu na fupi inamaana karibu vijana 700 wanaoweza kupokelewa na mpaka sasa tunao vijana 250 ambao wanategemea kufanya mtihani wa taifa ambao wa mwaka wa kwanza na mwaka wa pili.”amesema Thomas.

Amesema kuwa wanashuuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuweza kuwafadhili vijana na wasio na uwezo wapatao 109 ambao wanafadhiliwa kusoma kozi ya miezi sita na sasa hivi wanakwenda kuhitimu kozi hiyo na wamekuwa wakifundishwa kwa muda wa jioni.

Amesema Serikali imetoa shilingi bilioni 4.671 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa chuo hicho na pia imetoa shilingi bilioni 1.3 kwa ajili ya kununua vifaa na mitambo katika kalakana hivyo sasa hivi kalakana zimekamilika kwa asilimia kubwa.

Kwa upande mwanafunzi wa chuo hicho David Adam ambaye anasoma kozi ya muda mfupi (DMO) ambayo imedhaminiwa na ofisi ya Waziri Mkuu na mafunzo yao yameaza Juni6, mwaka huu na yanatarajia kumalizika Desemba 12, mwaka huu,na kozi hiyo ililenga mafunzo ya ufundi stadi wa kozi mbalimbali ikiwamo umeme,selemala,fundi magari,uwashi na ujenzi hivyo wanatoa shukrani kama Watanzania pamoja na ofisi ya Waziri Mkuu kwa kudhamini mafunzo hayo kwani wengine walikuwa hawana uwezo wa kugharamia mafunzo hayo.

Naye mwanafunzi Mungine Raines Oscar amesema kuwa yeye anasoma kozi ya Ukutubi kwa miwili na nusu hivyo wanampongeza kwa kazi kubwa anayoifanya na mwenyezi Mungu ambariki sana kwani anachokifanya anakwenda kugusa maisha ya Watanzania masikini.

Please follow and like us:
Pin Share