Na Mwandishi Maalumu – JKCI
Viongozi wa Serikali ya Nigeria wametembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa pamoja na kuangalia uwekezaji uliofanywa na Serikali katika matibabu ya kibingwa ya moyo nchini.
Ziara hiyo imefanyika hivi karibuni katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam baada ya viongozi hao kuwasili nchini kwaajili ya kuhuduria mkutano wa kujadili masuala ya ulinzi na usalama.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alisema baada ya viongozi hao kupata taarifa za huduma zinazotolewa JKCI waliweza kutumia fursa waliyoipata kufika JKCI na kujionea wenyewe huduma zilizopo.
“Ugeni wa viongozi wa serikali kutoka nchini Nigeria umetembelea maeneo mbalimbali ya taasisi yetu na kuangalia jinsi gani huduma za tiba ya moyo zinatolewa, ambapo tumewapitisha katika vyumba vya upasuaji wa moyo pamoja na kutembelea kliniki maalumu ya VIP”, alisema Dkt. Kisenge.
Dkt. Kisenge alisema viongozi hao wamefurahishwa na huduma zinazotolewa katika taasisi hiyo na kuahidi watakaporejea nchini mwao wataenda kuwa mabalozi wa kuwajulisha wagonjwa wa moyo kufika JKCI kwaajili ya matibabu.
“Baada ya kutembelea taasisi yetu wapo baadhi tumewapatia huduma na kuwafanyia uchunguzi wa magonjwa ya moyo na kuridhika na huduma zetu zinazotolewa katika kliniki maalumu ya VIP”, alisema Dkt. Kisenge.
Viongozi wa Serikali ya Nigeria wakiangalia video inayoonyesha huduma za kibingwa za matibabu ya moyo zinazotolewa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kiwete (JKCI) walipotembelea taasisi hiyo hivi karibuni kwaajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa pamoja na kuangalia uwekezaji uliofanywa na Serikali katika matibabu ya kibingwa ya moyo nchini
Mkurugenzi wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Tatizo Waane akipokea zawadi ya saa kutoka kwa kiongozi wa Serikali ya Nigeria wakati viongozi hao walipotembelea taasisi hiyo hivi karibuni kwaajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa pamoja na kuangalia uwekezaji uliofanywa na Serikali katika matibabu ya kibingwa ya moyo nchini.
Viongozi kutoka Serikali ya Nigeria na wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ziara yao ya kutembelea taasisi hiyo kwaajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa pamoja na kuangalia uwekezaji uliofanywa na Serikali katika matibabu ya kibingwa ya moyo nchini.