Viongozi wa dini msichoke kuwaunganisha watu – Biteko

#Atoa wito kujenga Taifa lenye umoja, upendo na mshikamano

Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dodoma

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko amewataka viongozi wa dini kutochoka kuunganisha watu ili kujenga Taifa lenye Umoja, Amani na Mshikamano

Mhe. Dkt Biteko ameyasema hayo kwenye Mkutano wa Baraza la Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste ambao ulikuwa na lengo la kuombea Amani na Umoja miongoni mwa makanisa hayo.

Amesema Serikali inathamini mchango mkubwa unatolewa na Viongozi wa Dini nchini na kutoa wito kwa maaskofu wa Makanisa ya kipentekoste kuunga mkono jitihada za serikali Kuhakikisha amani inadumishwa.

“Nawapongeza Sana Baraza la Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste kwa Kuwa na Umoja na waumini wengi nchini wanaofikia takrbani milioni 12, pamoja na Umoja wenye nguvu na mshikamano” amesema Dkt. Biteko.

Awali akizungumza kabla ya mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania-CPCT Askofu Dkt Barnabas Mtokambali, amesema Kuwa, viongozi wa dini wanathamini jitihada zinazofanywa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Kuhakikisha demokrasa, utawala Bora na Amani inadumishwa hapa nchini

“Tunaipongeza Serikali kwa kazi nzuri inayofanya kuhakikisha nchi iko kwenye utulivu, ustawi na amani na kuahidi kutoa ushirikiano pamoja na kuiombea Serikali

Mkutano wa Baraza la Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania ulianzishwa miaka thelathini iliyopita na ina jumla ya waumini milioni 12, na tayari madhehebu 28 yako mbioni kujiunga na Umoja huo wenye jumla ya Wanachama 128.

Mkutano huo wa Umoja wa Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste CPCT umehudhuriwa na Mwenyekiti wa kwanza wa Umoja huo Askofu Dkt. Sylvester Gamanywa, Makamu Mwenyekiti wa CPCT Askofu Dkt. Daniel Awet, pamoja na Maaskofu kutoka Madhehebu mbalimbali Chini ya Umoja huo.