Na Dotto Kwilasa, JamhuriMedia, Dodoma

Viongozi wa madhehebu ya dini wanaoteuliwa na kupatiwa dhamana ya kuongoza jamii wametakiwa kujiepusha na migogoro kutokana na madaraka yao,badala yake waisaidie serikali katika kuilinda amani na utulivu kama walivyoitwa kwenye nafasi zao.

Kaimu msajili wa Jumuiya Wizara ya Mambo ya Ndani Thomas Sanira amesema hayo kwenye ibada ya kuwasimika maaskofu wa tano wa Dayosisi iliyofanyika Kanisa la Free Angalican Church of Taanzania Mtakatifu Simoni Petro Usharika wa Ilazo Dodoma.

Sanira alisema kuwa migogoro mingi inayotokea kwenye taasisi za madhehebu ya dini inatokana na kugombea madaraka pamoja na mali,hali ambayo imekuwa ikiikosesha serikali kupata msaada wa kuwepo kwa amani na utulifu.

Alisema serikali moja ya sehemu kubwa ambao inategemea ni pamoja na eneo la taasisi za madhehebu ya kidini kutokana na mchango wake mkubwa wa kuhakikisha wanaiombea Nchi ikiwemo na amani na viongozi waliopo madarakani.

“Hivyo niwaombe maaskofu wa madhehebu ya dini wanaopewa dhamana ya madaraka kujiepusha na migogoro ambayo yaina tija,bali waifanye kazi waliyoiitiwa na Mungu ikiwemo na ukemeaji wa vitendo viovu ambavyo vimekosa uwepo wa maadili”alisema.

Aidha amewataka viongozi hao wa madhehebu ya dini kushirikiana na serikali katika kukemea vitendo vya ukiukaji wa maadili,ikiwemo kuinga mila na destuli za tamaduni za nje ambazo zimekuwa zikiwapoteza karibu vijana walio wengi.

Alisema kuwa kutokana na mila hizo za kutoka nje, viongozi wa madhehebu ya dini wanatakiwa kuhakikisha mnakemea vitendo hivyo ambavyo vimehadhiri baadhi ya vijana ambao Taifa linawategemea kwa siku zote.

Msajili huyo,pia amewataka waumini ndani ya madhehebu ya dini kutokuwa sehemu ya vyanzo vya mgogoro kwa viongozi ambao wanaowekwa madarakani,badala yake wapeni ushirikiano ili waweze kuifanya kazi walizoangizwa kuzifanya.

Awali akihubiri kwenye ibada hiyo Luyce Chimalusotola amewataka viongozi wa serikali kutoongopa kukemea na kuwachukulia hatua kwa wanaowaongoza pia wanapobainika kutowajibika kwenye nafasi zao kama walivyoteuliwa.

Alisema bado kuta tabia ya kulindana kwa baadhi ya viongozi mliopewa madaraka kwa wale ambao wapo chini yenu mnashindwa kuwaondoa hata kama wameharibu na kushindwa kufikia malengo yanayotakiwa kwenye maeneo yao na kwa jamii pia.

Pia alisema kuwa tabia hiyo ya kulindana inawagusa hata viongozi wakuu wa madhehebu ya dini baadhi yao wanashindwa kuwakemea.waumini wao kutokana na wengi wao kuna na mali na fedha ambazo wamekuwa wakipatiwa.
MWISHO.