Wana manyoya mithili ya manyoya ya paka na kwa ukaribu wanaonekana ni wazuri sana kuwachezea. Lakini amini usiamini, viwavi hao aina ya puss ni viumbe wasiopaswa kukaribiwa na binadamu hasa nchini Marekani.

Hii ni kwa sababu aina hiyo ya viwavi ndio wanaoongoza kwa kuwa na sumu kali nchini humo.

Kwa bahati mbaya, jamii hiyo ya viwavi walionekana huko Virginia mwezi Oktoba mwaka jana na kuzua mtafaruku mkubwa miongoni mwa wakazi wa maeneo hayo.

Jambo lililowatisha watu wengi ni kuwa utafiti uliofanyika ulionyesha kuwa viwavi hao hawakuibuka kwa bahati mbaya katika eneo hilo. 

Hadi muda huo viwavi hao walikuwa kama wakazi mahususi katika eneo hilo kwani walikuwa wameishi katika eneo hilo kwa miaka kadhaa na kuzoea mazingira yake.

Viwavi aina ya puss hawana uwezo wa kumrukia mtu na kumuuma. Lakini ngozi yao ya juu iliyofunikwa na manyoya ambayo ndiyo yanapaswa kukutia hofu.

Manyoya hayo yana sumu kali na iwapo yatakuganda mwilini, yanasababisha maumivu makali kama umeunguzwa moto. Baada ya muda yanasababisha mchubuko na maumivu mengine makali yanayoanza mara moja au si zaidi ya dakika tano baada ya kugusana nayo.

Baadhi ya watu walioguswa na manyoya hayo wanayafananisha maumivu yake sawa na maumivu yanayotokana na kuchomwa na kisu.

Ndio maana ushauri mkubwa unaotolewa na watalaamu ni kuwa unapomuoa kiwavi huyo usimkaribie kabisa. Wanasema unaweza kumwangalia kwa mbali lakini kamwe usithubutu kumgusa au kukaa pnade ambao upepo unaelekea kwani manyoya hayo yanaweza kupeperushwa na upepo na kukufikia.

Mkazi mmoja wa eneo hilo aliimbia CNN kuwa alipatwa na maumivu makali kama vile emechomwa kisu baada ya kugusa manyoya ya mdudu huyo.

Maofisa wa Idara ya Misitu katika eneo la Virginia jimboni Texas waliiambia CNN kuwa ilipokea taarifa kadhaa za kuonekana kwa viwavi hao.

Maofisa hao walisema taarifa hizo zilionyesha kuonekana kwa viwavi hao katika maeneo ya mashariki ya Virginia katika bustani za kupumzika na maeneo kama hayo. 

Mara moja maofisa hao wakaanza kutoa onyo kwa wakazi wa maeneo hayo kutowagusa wadudu hao kwani ni hatari kwa afya zao.

Katika Jimbo la Texas, viwavi hawa wanapatikana zaidi katika majita ya mwisho ya joto au mwanzoni mwa kipindi cha machipuo. 

Mara nyingi wanaonekana wakiwa katika miti yenye majani na vichaka karibu na nyumba za watu, shule, bustani za mapumziko na maeneo mengine ya nje.

Viwavi aina ya puss walioonekana Virginia katika Jimbo la Texas nchini Marekani.
597 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!