*Heche aingilia kati, asema CHADEMA itatoa tamko rasmi
Aziza Nangwa na Pendo Nguka, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Maneno machache yaliyotamkwa mkoani Iringa hivi karibuni yameibua mjadala, wadau wakitaka kujua ‘vyombo vya ulinzi na usalama ni mali ya nani?’
Kauli kwamba vyombo hivyo ni “mali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)” sasa imewafanya wanasiasa, wasomi, wanasheria na wanaharakati kuhoji mpaka unaotenganisha chama cha siasa, Serikali na taasisi za dola.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Idara ya Oganaizesheni, Paul Chacha, Septemba 26, mwaka huu, akiwa Iringa, alisema vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na viongozi wa Serikali ni mali ya chama hicho.
“Nani ambaye hajui vyombo vyote vya ulinzi na usalama ni mali ya CCM? Nani hajui mawaziri wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mali ya CCM? Nani hajui Waziri wa Ulinzi ni mali ya CCM?” alisema Chacha.
Kauli hiyo imezua mjadala kuhusu tofauti kati ya chama kilichoshinda uchaguzi na kuunda serikali, na umiliki wa taasisi za dola ambazo zinapaswa kuwahudumia wananchi wote.
Baadhi ya waliozungumza na JAMHURI wamesema chama kinachoshinda uchaguzi kinapata mamlaka ya kuunda na kuongoza serikali kwa kipindi kilichowekwa kisheria, lakini mamlaka hayo hayapaswi kutafsiriwa kuwa umiliki wa vyombo vya ulinzi na usalama.
Wengine wametaka viongozi wa juu kutoa ufafanuzi ili kuondoa mkanganyiko unaoweza kujitokeza miongoni mwa wananchi.
KWA HABARI ZAIDI SOMA GAZETI LA JAMHURI OKTOBA 6-12, 2026



