Na Helena Magabe,JamhuriMedia Tarime

NEMC kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkemia Mkuu Kanda ya Ziwa pamoja na Tume ya Madini Kanda ya Ziwa kwa udhamini wa Benki ya Dunia wametoa elimu ya matumizi salama ya zebaki kwa wachimbaji wa dhahabu zaidi ya 200 katika mgodi wa kibaga Tarime .

Mwezeshaji wa mafunzo hayo Musa Kuzumila ambaye ni Meneja wa usajili wa Kemikari na maabara za kemia ofisi ya Mamlaka ya maabara Mkemia Mkuu wa Serikali amesema zebaki ikiingia mwilini haitoki ni sawa virus vya ukimwi hivyo wachimbaji wanatakiwa kuchukua tahadhari kwa kujikinga wakati wa uchenjuaji na kuongeza kuwa kuchenjua ukiwa na kidonda au upele ni hatari zebaki itapenya na kuingia mwilini na kusababisha madhara.

Amesema njia salama za uchenjuaji ni kuvaa gloves,kuvaa maski na kuchenjua kwa kutumia kifaa cha kigida na vinginevyo ambavyo ni vya ghalama kwa wachimbaji wadogo ingawa vigida viko mbioni kutengenezwa na kuwafikia Wachimbaji na elimu hiyo imetolewa Kanda ya Ziwa Geita,Mwanza,Tarime,pamoja na Bunda.

Madhara ya moja kwa mtu aliyeathiliwa na zebaki ni pamoja kuathiri mfumo wa fahamu kwa kupoteza kumbu kumbu,kuharibika kwa mimba , kuzaliwa watoto wa utindio wa ubongo,kuathiri figo kusababisha msongo wa mawazo na matatizo mengineyo ya kiafya.

Akiendelea kuzungumza amesema kwa mujibu wa mradi unao ratibiwa na na baraza la hifadhi ya mazingira kufikia 2030 utumiaji wa zebaki utakoma na mbadara wa wa madini mengine ya kuchenjua dhahabu utakuwa umepatikana na kuongeza kuwa Dunia nzima ni wahanga wa zebaki wanatafuta mbadara .

Diwani wa Kata ya Kenyamanyori Farida Joel amesema changamoto ya uchenjuaji ipo kwani kina Mama wanalazimika kuchenjua bila kuvaa gloves kwa sababu gloves zikitumika hazikamati dhahabu ambapo amesema hata yeye aliwahi kuwa mchenjuaji huko Nyamongo ana uzoefu kuwa gloves haifai kwa uchenjuaji.

Amewaomba kina mama wanapokuwa wajawazito kusitisha kazi hiyo ili wasijifungue watoto wenye utindio wa ubongo kwani shule jirani ya Mtahuru ina kitengo cha watoto wa utindio wa ubongo,shule ya msingi Rebu pamoja na shule ya msingi Buhemba amesema kuna uwezekano kukawepo na Mahusiano ya zebaki.

“Elimu ilikuwa haijatolea mimi siwazuii kuchenjua ila nawaomba mtu akishakuwa mja zito aache kwa usalama wake na wa mtoto ndio maana hata kumekuwa na saratani mara za koo shule ya kirani hapa tu shule ya msingi Mtahuru kuna kitengo cha watoto wa utindio na Buhemba shule ya msingi hapa na Rebu shule ya msingi” alisema Farida.

Aidha ameomba maji yanayotiriri
katika eneo hilo kwa kukatiza barabara yapimwe ili kuhakikishiwa usalama wa hayo maji kwani watu hupita na kuyakanyaga wanafunzi,wengine huyatumia kuosha pikipiki,na wengine kunyweshea mifugo.

Tupeligwe Reuben kutoka ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Kanda ya Ziwa Mwanza amefundisha namna ya kutumia kigida ambacho ni kifaa salama na kinapunguza gharama za uchenjuaji kesni dhababu hujitenga na zebaki na zebaki inabaki na kutumika kwa wakati mwingine .

Mmoja wa washiriki wa mafunzo Joseph Mnanka (Master) amesema kina Mama wako kwenye hatari zaidi kwani wakati mwingine hujisahau na kula miwa kabla ya kunawa mikono au hujikuta wananunua matunda na kulaa hivyo hivyo bila kunawa kwa usahihi .

Kimito Marwa ameomba endapo vifaa salama vya uchenjuaji vitaingia mgodi wa kibaga uwe wa kwanza kupata vifaa hivyo pia amelalamikia juu ya mtu mmoja kutaka kujenga plant kwenye eneo la mwinuko akazuiliwa lakini anajenga kimya kimya lakini Diwani Pamoja na mtendaji wa Kata Fransins Macheo wamesema walishazuia ujenzi huo mpaka tararibu muhimu zifuatwe.

Mzee Nsenga Werema amohoji juu ya Tanzania kuwatokuwa na uwezo wa kuiomba China ambayo ndiyo mzalishaji wa zebaki hivyo kwa ugumu huo ameomba Nchi ibuni njia mbadala ya kabla ya kufika 2030 kwani sio mbali au kutumia sheking table na njia nyingine za uchenjuaji .

Mchenjuaji Debora Joseph ambaye anamiliki mwaro wake amesema amezoea kuchenjua kwa mikono ndio anakamata dhahabu na uchenjuaji huwa mgumu pale wananunua mawe magumu ambapo huosha kwa masaa mengi au kuosha siku mbili au wakati mwingine kazi huwa rahisi kutengemea na ulaini wa mawe na wakati mwingine hawapati kitu.