Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia

Jumuiya ya taasisi za kiislamu Tanzania wameishuku, Serikali kwa kutoa ushirikiano mkubwa katika suala la mtaala wa somo la dini ya kiislam na hatimaye kuliweka sawa.

Akizungumza na waandishi wa habari Amiri Mkuu wa Jumuiya ya Taasisi za Kislam Tanzania Alhaj Sheikh Musa Kundecha amesema baada ya kutoa malalamiko yao siku ya Agosti 10,2023 mwaka huu ,kueleza suala la serikali kumiliki mitaala wa somo la dini ya kislaamu na mambo yote ya imani yanayohusiana na dini yataondolewa.

Katika kuliweka sawa jambo hili waliomba kukutana na waziri mwenye dhamana,ili kulijadili sula hili kwa mustakabali maslahi ya nchi yetu alikubali tukakutana naye akiwa na wataalamu wake wa taasisi ya elimu.

“Tulikubalina suala la umiliki wa mitaala ya somo la dini, itabaki kwa wenye dini wenyewe kama ilivyokuwa zamani na serikali itashirikiana na wenye dini katika kuboresha mambo ya kitaalamu.

Kwa waislamu suala la dini na imani haviwezi kutenganishwa, kwani imani ndiyo msingi wa mafundisho ya dini.

Please follow and like us:
Pin Share