Hayo yamejiri Novemba 15, 2023 wakati Waziri wa Nchi Ofisi Rais TAMISEMI Mohamed Mchengerwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila alipokutana na wakazi hao katika viunga vya Ofisi za Young African Ilala Jijini Dar es Salaam

Akiongea na Wananchi hao Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI ametoa Kauli ya Serikali ya kuwalipa wakazi hao kuanzia kesho Novemba 16, 2023 ambapo hadi sasa asilimia zaidi ya 92 wameshahakikiwa wanasubiri kulipwa.

Mchengerwa amefafanua kuwa fidia itakayolipwa ni ya uthamini wa jengo na sio Ardhi, kwa mujibu wa sheria hawapaswi kulipwa fidia ya Ardhi kwa sababu wakazi hao wamejenga katika maeneo hatarishi lakini kwa upendo wa kipekee wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameelekeza kila mkazi wa eneo hilo atapewa kifuta jasho cha shilingi milioni 4 kiasi ambacho kiko nje ya fidia halisi ya Jengo.

Aidha Waziri wa OR-TAMISENI amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu amedhamiria kufanya Ujenzi wa kisasa wa barabara ya juu Jangwani ambayo inakwenda kuondoa kero ya mafuriko hivyo Ujenzi huo unakwenda sambamba na maboresho na uendelezaji wa Bonde la Mto Msimbazi kwa ujumla wake.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa anaoufanya katika Mkoa huo wenye masilahi mapana ya Umma ambapo amewataka wananchi na wakazi wa Bonde la Mto Msimbazi kutii Kauli ya Serikali kamywe wasirubuniwe wala kudanganyana Serikali inafanya uwekezaji Msimbazi kwa masilahi mapana ya watu wengi ” Mtu anakudanganya usisaini kuchukua fidia hiyo wakati yeye alishasini siku nyingi, mkitaka niwataje nitawataja” Amesema RC Chalamila