Na Helena Magabe, JamhuriMedia, Musoma

Waandishi wa Habari Mkoani Mara wametakiwa kuvaa mavazi maalum au beji wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao kwenye mazingira hatarishi.

Hayo yamesemwa katika mdahalo wa nne kati wa Jeshi la Polisi, waandishi wa Hlhabari, viongozi wa Dldini, asasi za kiraia, pamoja na Serikali kuhusu ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari.

Mdahalo huo uliofanyikia Musoma Mjini ambapo swala la vazi maalumu pamoja beji lilisisitizwa na wadau walioshiriki mdahalo huo kuwa ni muhimu sana.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara SSP Thomas Makene amesema ni muhimu Waandishi kuvaa mavazi maalumu au kuvaa beji zitazowatambulisha wakiwa kwenye majukumu yao kwenye mazingira hatari kama vile mikutano ya siasa na mandamano kuelekea kwenye uchaguzi.

Amesema sio rahisi kumtambua mwandishi akiwa hajavaa vazi la kumtamburisha wakati wa vurugu na kuomba waandishi ambao hawako kwenye klabu ya Waandishi Mara (MRPC) wajiunge ili wajue makubaliano hayo.

Aidha amesema mahusiano mazuri baina ya Polisi na waandishi yamekuwa imara baada ya kufanyika kwa midahalo iliyofanya daraja la kupunguza kuitirafiana na kuleta ushirikiano.

Wakili msomi Daudi Mahemba ambaye ni Mwanasheria wa Klabu ya Wandishi wa Mara (MRPC) ameichambua Ibara ya 18 ya Katiba ya mwaka 1977 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyofafanua kipengele cha habari.

Amesema ibara hiyo imefanyiwa marekebisho mara kwa mara na kufafanua kuwa inaeleza wazi juu ya uhuru wa kujieleza ,kutoa maoni,kupeana habari pamoja maelekezo ya utaratibu wa kisheria kwa wadau mbali mbali.

Amesisitiza weredi pande zote mbili na kwa upande wa Wandishi wanapohitaji habari kwa Jeshi la Polisi wazingatie mipaka yao ya kazi na taarifa ziwe na ukweli kwa maslahi ya umma na Taifa .

Habari hizo hazitakiwi kumbagua mtu kwa udini wake,ukabila zisishirikishe maslahi binafsi ya mwandishi ,zilinde vyanzo vya habari vya siri sambamba na mwandishi kutomtisha Mtu kwa kutaka habari toka kwake.

Mratibu wa haki za Binadamu Nimrod Swai ameshukuru UTPC pamoja IMS kuandaa midahalo hiyo ambayo italeta matokeo chanya na kusisitiza mavazi maalumu na kwamba ambaye hatavaa akipata matatizo asilaumu kwani kwa watu wengi kama huna vazi tofauti huwezi kujulikana kuwa ni Mwandishi.

Ameomba qaandishi wote wasajiliwe ili watambulike kwa wale ambao hawako kwenye klabu wajiunge na weredi uzingatiwe kwenye habari pamoja na kuandika habari zenye tija.

Kaimu Mwenyekiti wa Klabu ya Wandishi Mara Rafael Okelo amesema baada ya midahalo kufanyika imeleta matokeo chanya kwani Waandishi wameanza kuandika habari nzuri za Jeshi la polisi na kutolea mfano siku ya wanawake Duniani.

Amesema latika tafiti za hivi karibuni zilizofanywa na taasisi za kihabari nchini Tanzania zilibainisha kuwa waandishi wa habari kama sehemu ya jamii wanakumbana na madhila mbalimbali wanapofanya majukumu yao jambo ambalo linafanya Nchi yetu kuwekwa Katika orodha ya mchi ambazo bado zinamnyima uhuru wa Habari.

Mwenyekiti wa ACT Mkoa wa Mara, James Mnubi, amewata waandishi kukubaliana swala la kuvaa vazi maalumu kwenye mazingira yanayohatarisha usalama wao.

Amesema endapo mwandishi hapendi kuvaa kitambulisho kitakacho mtofautisha na watu wengine achukue tahadhari mwenyewe ya usalama wake.

Katibu Tawala Wilaya ya Musoma Mjini amesema Jukumu la Serikali ni kusimamia Amani usalama wa raia na mali zake Kwa hali hiyo tinapokuwa tunatekeleza majukumu yetu kila.moja anatakiwa kuzingatia uzalendo wa Nchi kwanza.

By Jamhuri