Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Morogoro

Wadau mbalimbali wa uhifadhi wameitaka serikali, kuongeza msukumo wa
kushirikisha jamii wakati wa mchakato wa uundaji sera mbalimbali.

Rai hiyo imetolewa na wadau mbalimbali wa uhifadhi ,walipokuwa kwenye mafunzo juu ya umuhimu wa jamii kujua haki ya kuishi kwenye mazingira safi, salama iliyoandaliwa na Shirika la Uhifadhi wa mazingira na Wanyamapoli duniani (WWF,) Morogoro.

Steven Kapinga ni mwezeshaji katika mafunzo hayo amesema ni vyema asasi za kiraia ,zikajikita katika utoa wa elimu kwa jamii itambue sheria ya haki ya kuishi kwenye mazingira safi na salama.

Kapinga amesema lengo la mafunzo hayo ni asasi kupaza sauti kwa jamii na kuona,inapata uelewa wa kutosha kupitia juu ya sheria hiiwa sababu haki hii bado ni mpya na watu wengi hawajaifahamu.

Tuna tarajia ujumbe utafika kwa watu wengi kutipa nyinyi, ili watu waweze kufahamu misingi na miongozo ya haki ya kuishi, kwenye mazingira safi na salama.

lakini pia wadau kuendelea kuongeza nguvu ya kupaza sauti , kwenye masuala kadhaa wa kadha yanayohusu mazingira ambayo yameonekana kuwa tishio kwa watu kuishi kwenye mazingira yaliyo safi na salama.

Tumeona makundi ya wanawake ,vijana na Watoto na kundi la watu
wanaoshughulika na masuala ya kijamii na wataalamu wa sera,mijadara yao mikubwa imejikita katika kuangalia zaidi changamoto zinazo zinazo zikumba makundi hayo.

Pia tumeona kwenye sera ndipo kwenye changamoto kubwa ,ambapo njia
bora ya kutengeneza ni kuhakikisha tuna kwenda kutekeleza yale ambayo
tumeona kama masuluhisho ya pamoja.

Mmoja wa wadau kutoka taasisi SUHODE Foundation Frank Luvanda amesema
Tanzania ina sera nzuri ,lakini baadhi zinahitaji uboreshaji na ushirikishwaji wa wadau na jamii ili kurahisha utekelezaji wake.

Luvanda amedai moja ya sheria inayohitaji maboresho ni ya uhifadhi, kwa sababu kutoa fidia kwa mkulima aliye athirika katika migongano ya ardhi kati ya binadamu na Wanyama pori ina mapungufu.

“Utagundua kuna changamoto kubwa kwenye upande wa fidia, hasa pale inapotokea wanyamapori wamekula mazao ya mkulima

Serikali inatoa fidia ndogo sana ukilinganisha na hali halisi ya kilichowekezwa kwenye shamba, mwishowe inasabasha chuki kwa uhifadhi na ndio chanzo kikuu cha Wanyama pori kuuwawa’’amesema.

Kwa upande mwingine amedai kuna mkinzano wa sheria zenyewe kwa zenyewe
,mfano sheria ya uhifadhi wa Wanyama pori 2009.

Inazuia shughuli zozote za kibinadamu kufanyika ndani ya hifadhi lakini sheria hiyo inaruhusu wawekezaji kuchimba Ulenium,mafuta na gesi asilia.

Ambayo Serikali imeyataja kwamba ni madini ya kimkakati, jambo ambalo sisi kama watu wa uhifadhi tunaona sio sahihi.

Kwa hiyo lazima tuchague wapi tunaweza kufanya hivyo, na wapi tunaacha kwa manufaa ya jamii ,kwa sababu baadhi ya sehemu zipo zimeachwa
kwa ajili ya kuongeza pato la taifa.

Sambamba na maboresho tunataka serikali kuweka chombo maalum cha kuratibu sera hizi ziweze kuleta maendeleo endelevu kwenye uhifadhi.

Kwa sababu changamoto ya ushiriki wa wadau kwenye kuunda, kutekeleza na kusimamia sera ,mara kadhaa imeonekana ni mchakato unao milikiwa na serikali na jamii wanakuwa wageni tu kwenye utekelezaji.

lakini kumbe ipo haja ya kuendelea kuyashirikisha makundi haya bila
kuyaacha, kwasababu itatusaidia sana kwenye utekelezaji wa sera zaidi
kwasababu ndiyo kundi kubwa linalohusika katika utekelezaji” alisema.

Happyness Ngonyani kutoka taasisi inayojishughulisha na elimu ya
mabadiliko ya tabia nchi na mazingira kwa wanawake na vijana Ifakara
,amesema moja ya changamoto zinazoikumba kundi hili ni uchafuzi wa
mazingira.

“Ambao upo katika taka ngumu na zenye maji, uzalishaji wa kelele,uchafuzi wa hali ya hewa kwenye mazingira yetu hivyo vyote
vinakosesha utulivu na kusababisha mlipuko wa magonjwa

Hivyo kama wadau tuna angalia ni jinsi gani tunaweza kutatua changamoto hii kwa pamoja, ili tuwe na jamii endelevu.

Ujenzi holela ,wafugaji kuhama hama, ,kilimo kwenye vyanzo vya maji, uchafuzi wa hewa ,shughuli za kiuchumi vyote vinachangia
ukiukwaji wa haki ya binadamu kuishi katika mazingira safi na salama.

Hivyo kama wadau ni vyema tukatoa elimu ya uhifadhi endelevu kwa jamii, ili kurudisha uoto wa asili kwa ajili ya kutunza mazingira na
kutunza afya zetu ziwe ubora.

Please follow and like us:
Pin Share