Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Morogoro

Shirika la Uhifadhi wa Mazingira na Wanyamapori (WWF), limewataka wadau wa uhifadhi nchini,kutoa elimu kwa jamii juu ya utekelezaji wa mkataba wa Kimataifa wa Biashara ya Wanyamapori, mimea iliyo hatarini kutoweka (CITES) kwa maendeleo endelevu ya viumbe hai.

Rai hiyo imetolewa Ofisa Sera na Uchechemuzi Maureen Mboka wa WWF kwenye mkutano na wadau mbalimbali wa uhifadhi nchini ulifanyika mkoani Morogoro.

Maureen amesema lengo kuu la warsha hiyo, ni kuwakusanya wadau kutoka katika makundi mbalimbali ya kijamii ,ili kupata uelewa wa mkataba wa CITES waweze kufahamu namna unavyofanya kazi mwishowe wawe mabalozi katika sehemu zao.

Amesema kuwa kupitia warsha hiyo wadau wameweza kutoa maoni mbalimbali, ambayo yataweza kujumuishwa katika mkakati wa pamoja wa utekekelzaji wa mkataba huo.

Amesema baada ya kuwajengea uwezo na kuelewa vizuri mkataba wa CITES unavyo fanya kazi, watakuwa chachu ya kuisadia Serikali kutokomeza biashara haramu ya wanyama pori.

“Elimu hii ikisambazwa katika jamii itasadia Serikali kuokoa Bioanuwai, ambazo ziko hatarini kutoweka na ambazo hazitakiwi kuuzwa kwa mujibu wa mkataba “amesema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET), John Chikomo, amesema warsha hiyo ni muhimu kwa wahifadhi ,kwa sababu imewasadia kuwajengea uwezo wadau juu ya namna gani mkataba wa CITES , unavyofanya kazi ili iwe rahisi kusadia kupambana na biashara haramu ya viumbe poli na mimea.

Chikomo amesema mkataba huo ni vyema kufahamika kwa jamii,kwasababu Tanzania ni moja kati ya nchi zilizolizia CITES hivyo baada ya mafunzo JET itawapatia mafunzo waandishi wengine juu ya mkataba huu.

“Kama wadau tuna jukumu la kusadia kueneza uelewa wa mkataba huu kwenye jamii, kuanzia ngazi ya chini mpaka juu Wananchi wanayo fursa ya kutekeleza mkataba huu ambao nchi imeridhia”amesema.

Frank Luvanda amesema mkata huo umelenga ushirikishwa jamii moja kwa moja ,katika suala zima la uhifadhi na kutoa maoni yao ili kuboresha utekelezaji wake na kulinda usalama wa bianuwai waliokuwepo kwa maendeleo ya kizazi kijacho.

Steven Kapinga ni mwezeshaji wa warsha hiyo amesema lengo la kuwakutanisha wadau wa uhifadhi pamoja, ni kujadili kwa undani mkataba huo ambao una husika na viumbe viumbe hai ,mimea na Wanyama.

Kapinga amesema mbali na kuwajengea uwezo ni kukusanya maoni ya mkataba , kupitia zile changamoto wanazopitia katika utekelezaji wa shughuli za uhifadhi.

“Matumaini yetu baada ya mkutano watakwenda kuwa wajumbe katika taasisi zao, wakati wa kutekelezaji mkataba huu kwenye jamii pia maoni yao waliokusanya yatakwenda kufanyiwa kazi na kuona jamii inashiriki kwenye utekelezaji wa mkataba.

Tunatarajia jamii kuwa na uelewa kuhusu mwenendo wa mkataba, pia watakuwa na ushiriki imara na thabiti wa kutoa maoni yao na kwenye utekelezaji wa sera’amesema.

Mkataba wa CITES umeweka mfumo wa utoaji maamuzi kuhusu utekelezaji wa mkataba kuanzia ngazi ya kamati za kitaalam kamati kuu na mkutano mkuu wa wanachama conference of parties.


Warsha inawasadia wadau kutambua mazao ya misitu na Wanyama poli ,ambayo hayaruhusiwi kufanyiwa biashara kimataifa na masharti maalumu ambayo yanawekwa kwa mujibu wa mkataba wa CITES kwa ajili ya kuwezesha biashara ya wanyamapoli .

Please follow and like us:
Pin Share