Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia,Mbeya

Watu watano wamekufa baada ya basi la Kyela Express kugongana uso kwa uso na basi dogo aina Toyota Coaster katika ajali iliyotokea mkoani Mbeya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ACP Benjamini Kuzaga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema kuwa ajali hiyo imetokea leo saa 2.30 katika kijiji cha Ibula Kata ya Kiwira.

Amesema kuwa ajali hiyo imetokea baada ya dereva wa Coaster ambaye amefariki kuendesha kwa mwendokasi kwa nia ya kutaka kulipita lori lililokuwa mbele yake na wakati huo basi la Kyela Express ambalo nalo lilikuwa kwenye mwendokasi likija mbele yake.

Mganga Mkuu wa Hosptali ya Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya, Diodes Ngaiza amesema, watu watano wamethibitika kufariki kutokanana na ajali huku majeruhi wakifikia 31.

Dkt.Ngaiza amesema kuwa kati ya majeruhi hao, 14 walikimbizwa katika hosptali ya Mission Igogwe, huku 17 wakikimbizwa katika hosptali ya Rufaa Kanda ya Mbeya (MZRH) kwa matibabu zaidi.