Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia

Kituo chama Wanahabari ,Watetezi wa Rasilimali na Taarifa MECIRA kimeamua kuwakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo, mazingira, uhifadhi na utalii kwa ajili ya kujadili umuhimu wa utunzaji wa vyanzo vya maji na uhifadhi wa mazingira.  

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar er Salaam, Mwemyekiti MECIRA, Habib Mchange, amesema kituo hicho kimeandaa kongamano hilo linalotarajiwa kufanyika Desemba 19 mwaka huu mkoani Iringa na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango.

Mwenyekiti Kituo cha Wanahabari ,Watetezi wa Rasilimali na Taarifa (MECIRA) Habib  Mchange akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kongamano  litakalo wakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo, mazingira, uhifadhi na utalii  kwa ajili ya kujadili umuhimu wa utunzaji wa vyanzo vya maji na uhifadhi wa mazingira.

“Tumeona ni jambokubwa kukutana na wadau pamoja wataalam ili kujadiliana na kuja na mawazo mbadala namna ya kuelimisha wananchi kudhibiti uharibu huo wa mazingira na vyanzo vya maji kwa sababu athari zake zinapokuja hazichagui itikadi ya mtu,’ amesema Habibu Mchange.

Atanabaisha kwamba kama MECIRA na Watanzania wote kwa ujumla, tuna wajibu wa kulinda mali zetu, tumeona kwamba tukiendelea kusubiri serikali pekee ifanye huku tumekaa tukiangalia hali hii ya uharibifu wa mazingira inaendelea kama ilivyo sasa, tutajikuta tunaendelea kulaumu tu huku athari ikiongezeka,”alisema Mchange.

Mdau wa masuala ya uhifadhi Bw. Jackton Mayerere akifafanua mambo mbalimbali kuhusu kongamano  litakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo, mazingira, uhifadhi na utalii  kwa ajili ya kujadili umuhimu wa utunzaji wa vyanzo vya maji na uhifadhi wa mazingira.

“Kwa hiyo, tumeamua kuchukua hatua badala ya kuwa sehemu ya wanaolalamika, tutumie taaluma zetu kubadili mitizamo ya wananchi kuhakikisha inaamka na inashiriki katika kuhifadhi, kutunza na kutetea rasilimali zake.”

“Tunataka mwananchi anayelima kwa mfano kandokando ya Mto Ruvu au Ruaha ambaye huenda hajui kwamba anaharibu mazingira, ajue sasa. Kwa hiyo sisi kama wanahabari tutafanya kazi hiyo kwa kushirikiana na wataalam wa mazingira, kilimo, mifugo, kuwaonyesha kwamba ni namna gani wanatakiwa wawaambie wananchi kwamba katika eneo fulani hawatakiwi kulima na sehemu gani hawatakiwi kuingiza mifugo badala wafanye nini.”

“Tunataka tuwe wanahabari ambao kupitia kazi zetu tunaleta tija katika jamii na taifa letu kwa kutoa elimu iliyo sahihi juu ya suala hili, nchi yetu ni miongoni mwa mataifa yanayoumia sana na suala la uharibifu wa mazingira, tushirikiane tutengeneze uelewa kwa wananchi” amesema.

Khamis Mkotya mkuu wa Mawasiliano Taasisi ya MECIRA akitoa maelezo kadhaa kuhusu kongamano hilo.

Ofisa Mawasiliano wa MECIRA, Hamisi Mkotya, alisema wanahabari wana wajibu wa kupaza sauti kusemea jambo hilo kama ambavyo wamekuwa wakifanya katika mambo mengine ili kupambana na uharibifu huo wa mazingira na vyanzo vya maji.

“Unapoharibu mazingira au vyanzo vya maji, haumkomoi mtu, unajikomoa wewe mwenyewe. Kuna shughuli za binadamu zinafanyika kiholea au isivyo halali na kuharibu mazingira na vyanzo vya maji. Kuna kilimo kinafanyika kiholea, ufugaji wa kuingiza mifugo katika maeneo ambayo hayaruhusiwi, kwa hiyo yote hayo, rasilimali zinavyoharibika, taifa linapata hasara, lakini tunaathirika sisi sote.

Mdau wa Uhifadhi,Manyerere Jackton, amesema ni wajibu wa wanahabari kujipambanua badala ya kuwa sehemu ya watu wanaolalamika, kutumia kalamu zao kuelimisha umma juu ya umuhimu wa kutunza mazingira hayo.

Baadhi ya maofisa wa MECIRA wakiwa katika mkutano huo.

“Mazingira yanapo athirika hayachagui mtu, sisi wote tunaathirika. Leo hii kuna mgawo wa umeme, watu wote wanaathirika bila kujali itikadi ya mtu, kwa hiyo tumeona sisi kama wanahabari tulete mabadiliko chanya katika suala hili la kutunza na kuhifadhi mazingira yetu kwa sababu tunao wajibu huo wa kushirikiana na serikali kuelimisha jamii,”amesema Manyerere.

By Jamhuri