Na Suzy Butondo, Jamhuri Media, Shinyanga

Watoto watatu wa familia mbili tofauti wamefariki dunia katika kijiji cha Zongomela kata ya Zongomela katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga baada ya kuangukiwa na kuta za nyumba waliyokuwemo kutokana na mvua zilizokuwa ziendelea kunyesha, huku mmoja mwenye umri wa miaka minne akinusurika kifo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi, amesema tukio hilo limetokea jana Januari 10, 2024 saa 11 alfajiri katika Kata ya Zongomela Manispaa ya Kahama.

Magomi amewataja watoto waliopoteza maisha kuwa ni Shija Mihayo mwenye umri wa miaka (5), Matha Shaban mwenye umri wa miaka (7) na Maguzu Shija mwenye umri wa miaka (5).

Magomi amesema vifo hivyo vimesabishwa na mvua kubwa iliyokuwa ikiendelea kunyesha na kulowanisha kuta za nyumba hiyo na kusababisha kuanguka.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi.