KARIBU watu 100 wamekufa nchini India katika siku za karibuni kutokana na joto kali lililolikumba taifa hilo.

Watu hao wamekufa katika majimbo mawili yenye idadi kubwa zaidi ya watu ya Uttah Pradesh lililoko magharibi mwa nchini hiyo na Bihar, lililopo upande wa mashariki, huku maafisa wakiwataka wakazi na hasa wa miaka 60 na zaidi na wenye maradhi mbalimbali kukaa ndani nyakati za mchana.

Kulingana na mamlaka, waliokufa ni wazee wa zaidi ya miaka 60 na wenye matatizo ya kiafya, na huenda joto kali lilichochea vifo vyao.

Afisa wa afya katika eneo la Ballia S.K Yadav amesema karibu watu 300 walilazwa katika hospitali ya wilaya siku tatu zilizopita kwa maradhi yaliyochochewa na joto kali.

By Jamhuri