Takriban watu 26 wamekufa na wengine kadhaa haijulikani walipo kufuatia ya ajali ya boti hapo jana katika eneo la Mokwa kaskazini mwa Nigeria.

Msemaji wa Gavana wa Jimbo hilo la Niger Bologi Ibrahim amesema boti hiyo ilikuwa na watu zaidi ya 100, wakiwemo wanawake na watoto.

Viongozi wa eneo hilo wamesema watu wengine 30 wameokolewa, huku wakibaini kuwa ajali hiyo mbaya zaidi kushuhudiwa jimboni humo katika kipindi cha miezi mitatu. Kupakia watu kupita kiasi na utunzaji duni wa vyombo hivyo vya usafiri ndio sababu kuu ya ajali za mara kwa mara nchini Nigeria.

Mwezi Julai, zaidi ya watu 100 walikufa wakati mashua iliyojaa kupita kiasi ilipopinduka katika jimbo la Niger, ikiwa ni mojawapo ya janga kubwa zaidi katika miaka ya hivi karibuni

By Jamhuri