Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar

Watu 604 wamepata huduma za upimaji na matibabu ya moyo wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo duniani yaliyofanyika katika Hospitali ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group iliyopo Temeke jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi wa JKCI Hospitali ya Dar 99Group Dkt. Tulizo Shemu alisema upimaji huo ulifanyika kwa muda wa siku mbili ambapo wananchi walipata huduma za upimaji, ushauri pamoja na kupewa dawa kwa wale waliokutwa na matatizo.

Dkt. Shemu alisema mwitikio wa wananchi ulikuwa ni mkubwa na kuwaomba wananchi wakati mwingine watakaposikia kuna upimaji wa magonjwa mbalimbali unafanyika mahali wasiache kwenda kupima afya zao.

”Watu 604 walifanyiwa vipimo vya awali vya magonjwa ya moyo kati ya hao 99 walifanyiwa vipimo vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi pamoja na mfumo wa umeme wa moyo na 58 tumewakuta na matatizo ya moyo yanayohitaji matibabu ya kibingwa tumewapa rufaa ya kuja kutibiwa JKCI”,

Madaktari  wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakizungumza na  wananchi waliofika  JKCI Hospitali ya Dar Group kwaajili ya kupata huduma ya upimaji na matibabu ya  moyo wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo duniani. 

 “Wagonjwa wengi tumewakuta na tatizo la shinikizo la juu la damu na wengine wameshapata madhara ya shinikizo la damu hii ikiwa ni pamoja na kutanuka kwa misuli ya moyo, wengine mishipa yao ya damu ya moyo imeziba,  kuna ambao tumewakuta na kiwango kikubwa cha mafuta kwenye damu pamoja na matatizo mengine ya moyo”, alisema Dkt. Shemu.

Dkt. Shemu alisema gharama za matibabu ya moyo ni kubwa na kwa asilimia 80 magonjwa hayo yanaweza kuepukika njia moja wapo ya kuyaepuka ni kufanya mazoezi na kupima afya mara kwa mara ili kujua kama unamatatizo ya moyo na kuanza matibabu mapema kuliko kusubiri wakati ambao moyo umepata shida na kuanza matibabu.

Moyo Tanzania (TCS) Robert Mvungi akisikiliza mwananchi aliyefika  JKCI Hospitali ya Dar Group kwaajili ya kupata huduma ya upimaji na matibabu ya  moyo wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo duniani. Watu 604 walipata huduma za matibabu kati yao 99 walifanyiwa vipimo vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi na mfumo wa umeme wa moyo na 58 wanahitaji  kupata matibabu ya kibingwa.

Kwa upande wake aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Mhe. Mobhare Matinyi aliyeongoza matembezi ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza alisema wilaya hiyo imejipanga kuhamasisha jamii kufanya mazoezi na kupima afya ikiwa ni njia moja wapo ya kupambana na magonjwa hayo  yakiwemo ya moyo.

“Leo hii vikundi mbalimbali vya mazoezi vimetembea umbali wa kilomita nne kutoka uwanja wa Uhuru hadi Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) hospitali ya Dar Group kwa ajili ya kufanya mazoezi. Ninaipongeza JKCI kwa kusherehekea siku ya moyo duniani kwa kufanya upimaji wa afya na kuandaa matembezi haya”,

Afisa Utafiti na Mafunzo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Zabela Mkojera akichukuwa taarifa za mwananchi aliyefika JKCI hospitali ya Dar Group kwaajili ya upimaji na matibabu ya moyo wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo Duniani yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

“Licha ya kuhamasisha jamii kufanya mazoezi Wilaya ya Temeke pia inahamasisha wananchi kufanya usafi katika mazingira yao, kupima afya  na  katika matukio makubwa yanayofanyika tunawahamasisha wananchi kuchangia damu na mwitikio huwa ni mkubwa”, alisema Mhe. Matinyi.

Matinyi alimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha katika sekta ya afya ambapo sasa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inauwezo wa kuwahudumia watanzania na wagonjwa kutoka nje ya nchi na kuwaomba wananchi waitumie hospitali hiyo katika matibabu.

 Nao wananchi walioshiriki zoezi la upimaji na matibabu hayo ambayo yalienda sambamba na matembezi ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza  waliishukuru Serikali kwa huduma waliyoipata na kusema imewasaidia kupata elimu na matibabu  ya magonjwa ya moyo.

“Mimi ninashida ya presha nilisikia katika taarifa ya habari kutakuwa na huduma ya upimaji nami nikaamua kuja kupima ili nione maendeleo ya afya yangu, nashukuru sana nimepima na nimepewa dawa za kutumia huduma hii nimeipata bila malipo yoyote yale”,.

“Huduma niliyoipata ni nzuri, ninaomba huduma hii iweze kwenda hadi vijijini ili wananchi  wengi wanaoteseka na magonjwa ya shinikizo la damu na moyo ambao  uwezo wao kifedha ni mdogo waweze kufaidika nayo”, alishukuru Christina Mohamed mkazi wa Gongo la Mboto.

“Mimi sina bima ya afya nilikuja na mama yangu kupima afya namshukuru Mungu sina tatizo lolote lile la moyo ila nimekutwa na matatizo mengine nimepewa dawa za kikohozi na mafua , ninawashauri wananchi wenzangu nao waje kupima afya zao kwani huduma inatolewa bila malipo yoyote yale”, alisema Emmanuel Babu mkazi wa Tabata.⁹

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Mhe. Mobhare Matinyi akiongoza matembezi ya kuhamasisha jamii kufanya mazoezi na kupima afya ikiwa ni njia moja wapo ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo. Matembezi hayo ya umbali wa kilometa nne yalifanyika hivi karibuni kuanzia  uwanja wa Uhuru hadi Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) hospitali ya Dar Group.

Kikundi cha Wasafi Jogging wakiwa katika  matembezi ya kuhamasisha jamii kufanya mazoezi na kupima afya ikiwa ni njia moja wapo ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo. Matembezi hayo ya umbali wa kilometa nne yalifanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam kuanzia  uwanja wa Uhuru hadi Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) hospitali ya Dar Group.

Baadhi ya Askari wa Jeshi la Polisi wakiwa katika  matembezi ya kuhamasisha jamii kufanya mazoezi na kupima afya ikiwa ni njia moja wapo ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo. Matembezi hayo ya umbali wa kilometa nne yalifanyika hivi karibuni kuanzia  uwanja wa Uhuru hadi Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) hospitali ya Dar Group.

Baadhi ya wananchi waliopata huduma ya upimaji na matibabu ya moyo wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo Duniani yaliyofanyika hivi karibuni katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) hospitali ya Dar Group wakipewa dawa za kutibu maradhi mbalimbali waliyokutwa nayo. Watu 604 walipata huduma za matibabu kati yao 99 walifanyiwa vipimo vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi na mfumo wa umeme wa moyo na 58 wanahitaji kupata matibabu ya kibingwa

.

Afisa Utafiti na Mafunzo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Loveness Mfanga akichukuwa taarifa za mwananchi aliyefika JKCI hospitali ya Dar Group kwaajili ya upimaji na matibabu ya moyo wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo Duniani yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Afisa Utafiti na Mafunzo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Maclina Komba akichukuwa taarifa za mwananchi aliyefika JKCI hospitali ya Dar Group kwaajili ya upimaji na matibabu ya moyo wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo Duniani yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es amalgam.

By Jamhuri