Wawili washikiliwa kwa tuhuma za mauaji ya mwanafunzi Dodoma

Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dodoma

Wakazi wawili wa mkoani Dodoma wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za mauaji ya mwanafunzi wa shule ya msingi Mtumba, Farida Makuya (16) ambaye alitakiwa kufanya mitihani jana.

Inadaiwa alipigwa na kitu kizito kichwani wakati mama yake akifanya biashara katika klabu cha pombe.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma (RPC), Martin Otieno wanafunzi amesema kuwa mwanafunzi huyo aliuawa usiku Jumanne, Oktoba 4, 2022 nyumbani kwao Mtumba jijini Dodoma na watu wasiojulika.

Inadaiwa alipigwa na kitu kizito kichwani wakati mama yake akifanya biashara katika klabu cha pombe.

Kamanda Otieno amesema jeshi hilo linawashikilia watu wawili kwa mahojiano lakini msako zaidi unaendelea kwani tukio hilo ni baya ambalo haliwezi kuvulimika kwani kitendo kilichofanyika kwa binti huyo ni cha kinyama kinachopaswa kulaaniwa.