Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi (Mb.), amewasili mkoani Shinyanga kwa ziara ya kikazi na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, leo Julai 27, 2026.
Akiwa mkoani humo, Waziri Ndejembi ataongoza viongozi na wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kushuhudia utiaji saini wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa jua chenye uwezo wa Megawati 100, awamu ya pili, katika eneo la Ngunga, wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.
Waziri ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Felchesmi Mramba, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Subira Mgalu (Mb.), pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Simon Songe Lusengekile.












