Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limeonya kuwa zaidi ya watu 3,500 hufariki kutokana na virusi vya homa ya ini kila siku na kuongeza idadi ya wanaoathirika duniani.

Shirika la afya duniani limesema zaidi ya watu 3000 hufariki kwa homa ya ini kila siku
Picha: magicmine/Zoonar/picture alliance.

Kulingana na ripoti ya WHO iliyotolewa sanjari na Mkutano wa Kilele wa Ugonjwa wa homa ya Ini utakaofanyika nchini Ureno wiki hii, Takwimu mpya kutoka nchi 187 zimeonyesha kuwa idadi ya vifo ilipanda hadi watu milioni 1.3 mwaka 2022 kutoka milioni 1.1 mwaka 2019.

Licha ya kwamba kuna dawa za kawaida na za bei nafuu ambazo zinaweza kutibu virusi hivyo, ripoti ya WHO inasema asilimia tatu tu ya walioambukizwa homa sugu ya ini walipokea matibabu ya kuzuia virusi hivyo kufikia mwisho wa 2022.

Afrika inachangia asilimia 63 ya maambukizo mapya ya ungojwa huo, huku mtoto mmoja tu kati ya watano akipata chanjo wakati wa kuzaliwa katika bara hilo.

By Jamhuri