Bohari ya Dawa leo imekabidhi bidhaa za afya mbalimbali kwa waathrika wa mafuriko Wilayani Rufiji mkoani Pwani.

Bidhaa hizo zimekabidhiwa kituo cha Afya Mohoro kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji ambazo ni pamoja na Dawa, za kuzuia na kutibu malaria, kuhara na yale ya mlipuko kama vile kipindupindu.

Kwa upnde wa vifaa tiba ni pamoja na magodoro, mashuka na vyandarua, milingoti ya kutundikia maji tiba ( Drip Stand), Binliners na vifaa vingine vitakavyosaidia katika zoezi hili.

Akizungumza wakati wa kukabidhiwa bidhaa hizo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Dr. Hamis Abdallah. ameishukuru MSD kwa juhudi za haraka zilizofanyika kuweza kuwafikia wahanga wa mafuriko. Ameongeza kuwa bidhaa hizo zitasaidia katika utoaji wa huduma kwa waathirika wa mafuriko.

Naye meneja wa MSD Kanda ya Dar es Salaam Betia Kaema amesema MSD baada ya kuona taarifa ya janga hili iliamua kuchukua hatua za haraka ikiwemo kuwasiliana na mamlaka za Wilaya ili kufahamu mahitaji yanayotakiwa kwa waathirika. “Leo tumekabidhi vifaa ili kuhakikisha huduma za afya hazisimami kwa wananchi, lakini pia tumetembelea maeneo mbalimbali kujionea hathari za mafuriko haya.MSD itaendelea kutoa ushirikiano mpaka pale hali itakapotengamaa.” Alisema Betia