Serikali imewachukulia hatua watumishi wa wawili wa afya ambao video yao ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikiwaonyesha watumishi hao wakijibizana kuhusu matumizi ya vifaa (vitendanishi) vya kupimia malaria vilivyoisha muda wake wa matumizi.

Watumishi hao Rose Shirima ambaye ni mkunga na Getogo James Chuchu (Mteknolojia wa Maabara) ambao ni wafanyakazi wa zahanati ya Ishihimulwa iliyoko Halmashauri ya Utyui mkoani Tabora ambao wamefikishwa kwenye mabaraza yao ya kitaaluma kujibu tuhuma hizo.

Mnano Januari 6,2023 ilisambaa video iliyozua taharuki kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo mtandao wa WhatsApp ikiwahusisha watumishi hao wawili wakijibizana kwa kutumia lugha isiyo na staa kuhusu matumizi ya vifaa violivyoisha muda wake.

TAZAMA VIDEO HIYO HAPA

By Jamhuri