Serikali kufuatilia video ya mhudumu wa afya Tabora iliyosambaa mtandaoni

Kufuatia kusambaa kwa video fupi katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha mhudumu wa afya akijibizana na mwenzake, huku mmoja akipinga matumizi ya vifaa tiba vilivyokwisha muda wake wa matumizi.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametoa taarifa kuhusu video hiyo kuwa Timu ya Usimamizi Afya ya mkoa wa Tabora wanafuatilia suala hilo na hivyo serikali itatoa taarifa juu ya hatua zitakazochukuliwa

“Kuhusu suala hili – Timu ya Usimamizi Afya ya Mkoa (RHMT) wa Tabora na ya Halmashauri (CHMT) ya Wilaya ya Uyui wanafuatia suala hili.
Serikali itatoa Taarifa kwa umma juu ya hatua zilizochukuliwa. Tunawashukuru wote walioibua suala hili”amesema

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa kuna vitandanishi vya kupimia malaria ambavyo havijaisha muda wake vitakavyotosheleza kwa matumizi ya miezi sita


“Aidha niongeze kuwa nchi yetu ina stock ya vitendanishi vya kupima malaria (MRDT) ambavyo havija-expire vya kutosheleza miezi 6.”amesema