Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Salome Makamba leo, Octoba 21, 2026, amewasilisha mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Subira Mgalu utekelezaji wa bajeti ya Wizara katika robo ya kwanza wa mwaka wa fedha wa Serikali wa 2026/27 sekta ndogo ya Umeme na Nishati Jadidifu.
Kikao hicho kimefanyika katika Kumbi za Bunge Jijini Dodoma, ambapo Wizara ya Nishati imewasilisha utekelezaji wa Bajeti ya Wizara katika maeneo mbalimbali ikiwemo, utafiti, uzalishaji, na matumizi ya nishati ya umeme inayozalishwa na vyanzo jadidifu na mbadala vinavyopatikana nchi.
Pia utekelezaji wa mradi wa kupeleka umeme vitongojini awamu ya pili A na B (HEP IIA NA HEP IIB), utekelezaji wa mradi wa gridi imara, utekelezaji wa miradi ya nishati safi ya kupikia, pamoja na utekelezaji wa Bajeti ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Kikao hicho kimehudhuriwa na Wajumbe wa Kamati, Katibu Mkuu anayeshughulikia Umeme na Jadidifu Wizara ya Nishati, Mha. Felshesmi Mramba, Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Nishati Ndg. Petro Lyatuu, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Ndg. Lazaro Twange, na Mkurugenzi Mtendaji wa REA Mha. Hassan Saidy, Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Taasisi zake.












