Na Tatu Saad Jamhuri Media

Klabu ya Yanga inatarajia kuingia dimbani kukabiliana na klabu ya Real Bamako ya huko Mali katika mchezo wao wa marudiano wa Kundi D wanaloshiriki katika kombe la shirikisho Afrika.

Yanga wataminyana na Real Bamako kesho saa moja usiku katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam kufikisha idadi ya michezo minne ya kombe hilo.

Akizungumzai maandalizi yao juu ya mchezo huo kocha mkuu wa Yanga Sc Nasreddine Nabi amesema yeye kama kocha amerekebisha makosa yote ambayo aliyaona katika mechi zilizopita hivyo amewaandaa vyema wachezaji wake kukabiliana na Real Bamako na kuchukua alama tatu.

“Kuna makosa mengi hali hiyo kesho katika mechi zilizopita, nayo tumeyarekebisha hivyo tunategemea kesho kuwa na utimamu mkubwa katika mchezo wa kesho”. Alisema Nasreddine Nabi.

Naye mchezaji wa Yanga Sc amesema wao kama wachezaji wana morari kubwa na mchezo wa kesho ili kuhakikisha wanapata ushindi.

“Sisi Kama wachezaji tumejipanga vizuri na tuna morari kubwa dhidi ya mchezo wa kesho kuhakikisha tunapata ushindi wa alama tatu.

Hata hivyo Nabi alisema kuwa tatizo lililojitokeza katika mechi zao zilizopita kwa kufungwa mabao yote kwa njia ya kona wamelidhibiti vizuri kwani tatizo ilikua ni mawasiliano madogo kwa wachezaji wenyewe wakati wa kuzuia mpira wa kona na sio ufupi wa mabeki kama Inavyosemekana.

Mechi ya mwisho Yanga na Real Bamako walitoka sare ya bao 1-1 katika uwanja wa Stade Du 26 Mars huko nchini Mali, ambapo Bamako walifanikiwa kusawazisha dakika za mwisho.

By Jamhuri