Yanga yashindwa kufurukuta mbele ya USM Alger

Klabu ya Yanga imeshindwa kufurukuta mbele ya wapinzani wao USM Alger ya nchini Algeria baada ya kuokea kichapo cha mabao 2-1 kwenye mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Licha Yanga kuutawala mchezo katika kipindi cha kwanza waliruhusu bao la mapema kupitia kwa mshambuliaji Aymen Mahious dakika ya 32 ya mchezo,bao ambalo liliwapeleka mpumziko USM Alger wakiwa mbele 1-0.

Kipindi cha pili Yanga iliendelea kutengeneza nafasi nyingi kwaajili ya kusawazisha bao bila mafanikio hivyo kocha akalazimika kufanya mabadiliko ambayo yalizaa matunda kwa kuwaingiza baadhi ya wachezaji wakiwemo  Morisson, Salum Aboubakar, Djuma Shaban na Lomalisa Mutambala ambapowaliweza kupata bao la kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wao Fiston Mayele, goli likitengenezwa na Morisson dakika ya 82.

Baada ya Yanga kupata bao, USM Alger waliweza kuongeza bao dakika mbili mbele kupitia kwa nyota wao Islam Merili dakika ya 84.