Timu ya Yanga SC imetinga raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa barani Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Zalan FC kutoka Sudan Kusini mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa katika uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Kipindi cha kwanza timu zote zilienda mapumziko bila kufungana huku Yanga wakiwa wameutawala mchezo huo.

Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kulishambulia lango la Zalan FC kama nyuki mnamo dakika ya 47 Farid Mussa alianza kufungua ukurasa wa mabao akifunga bao safi.

Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Burkina Faso Stephanie Aziz Ki aliwanyanyua mashabiki wa Yanga dakika ya 56 akifunga bao safi lililoenda moja kwa moja na kumuacha mlinda mlango wa Zalan FC.

Mshambuliaji hatari kwa sasa Fiston Mayele alipiga hat-trick yake ya pili baada ya kufunga mabao dakika ya 59,62 na 66,ikumbukwe mchezo wa kwanza Mayele alipiga hat-trick.

Kwa ushindi huo Yanga wametinga hatua hiyo kwa jumla ya mabao 9-0 baada ya mchezo wa kwanza kufungwa mabao 4-0 na wanamsubiri mshindi kati ya St.George ya Ethiopia au Al Hilal Omdurman kutoka Sudan.

Wawakilishi wengi katika Kombe la Shirikisho barani Afrika timu ya Kipanga kutoka Zanzibar imetinga hatua ya raundi ya kwanza baada ya kushinda kwa Penalti 5-4 dhidi ya Al Hilal Wau.

Licha ya Geita Gold FC kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Al Sahil wameshindwa kufuzu raundi ya kwanza kwa bao la ugenini badaa ya mechi ya kwanza kufungwa bao 1-0.

Simba watashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kesho kucheza na Big Bullet kutoka Malawi mchezo wa Kwanza Simba waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 hivyo wanahitaji sare au ushindi na kusonga mbele katika Michuano hiyo.

Please follow and like us:
Pin Share