Na Jumanne Magazi, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Kampuni ya Dowei Care Technology ambao ni wazalishaji wa Taulo za kike na za watoto (SOFTCARE) wanatarajia kutoa msaada wa bidhaa zao katika Hospital ya Taifa ya Muhimbuli katika kitengo cha huduma za mama na mtoto lengo likiwa kuendelea kumsaidia mwanamke kujisitiri pindi anapokuwa kwenye siku zake za hedhi.

Akizungumza leo Machi 21,2024 jijini Dar es Salaam wakati wakisaini mkataba mpya na balozi wa bidhaa hizo ambae ni mfanyabiashara maarufu Zarina Hassan(Zari the boss lady) Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Victor Zhang amesema wamekuwa wakipata matokeo chanya na yenye tija kutokana na uwepo wa boalozi huyu.

Amesema kampuni yao wamekuwa wakirudisha faida kwa jamii kwa kushiriki kampeni nyingi za kitaifa ikiwa ni pamoja na ugawaji wa taluo za kike kwa mabint wa shule za msingi na sekondari.

“Tumekuwa tukipata matokeo chanya kwa kumtumia huyu balozi wetu lakini pia kutokana na mtokeo hayo tumekuwa na utaratibu wa kurudisha faida kwa jamii tunawapunguzia mzingo mabint kwa kukosa taulo za hizo jambo ambalo linawasababishia kukosa masoma pindi wanapokuwa kwenye hedhi zao”,Amesema Zhang

Akizungumzia kufanyakazi na balozi huyo amesema wameamua kuendelea na kufanyakazi na Zari kwa maana ameweza kuleta matokeo chanya kwa kampuni yao kwani wamezidi kupata faida.

Kwa upande wake Zarina Hassan ameishukuru kampuni hiyo ya Dowei kwa kumpa mkataba mwingine tena mnonno huku akiahidi kuendelea kuwasaidia wanawake na watoto wanaoshindwa kupata huduma ya taulo hizo kutokana na kuwepo kwenye mazingara magumu.

“Nitahakikisha bidhaa hizi zinafika kwa watu maskini na wenye uhitaji hususani wanawake na watoto wa kike ambao wanaishi kwenye mazingira magumu”,Amesema Zarina.

By Jamhuri