Daily Archives: June 25, 2019

Mwenyekiti CWT adanganya

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Clement Mswanyama, amewadanganya walimu na Watanzania kwa ujumla juu ya umiliki wa mali za walimu, JAMHURI linathibitisha. Hivi karibuni, Mswanyama ameitisha mkutano na waandishi wa habari jijini Dodoma na bila aibu akawaambia uongo kuwa Chama cha Walimu Tanzania kinamiliki hisa 99 za Kampuni ya Teachers Development Company Limited (TDCL), ...

Read More »

Posta na fikra za analojia!

Mabadiliko ya ulimwengu wa leo yamemfanya Mpita Njia (MN) naye aishi kulingana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia. Ni kwa sababu hiyo, naye amejikuta analazimika kujua namna ya kuingia kwenye mitando na ‘kuchati’ japo kasi yake si kama ya wenye ulimwengu wa sasa, yaani vijana. Mpita Njia ingawa ana umri mkubwa, amejitahidi kuwa memba kwenye makundi mengi ya whatsapp na mengine mengi. ...

Read More »

Mapya vitambulisho vya ujasiriamali Kwimba

Vitambulisho vya Rais John Magufuli vya wajasiriamali vimezua sokomoko baada ya kaya maskini zilizomo kwenye mpango wa kusaidiwa fedha kutoka katika Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini (TASAF) kuamriwa kulipia vitambulisho hivyo. Hali hiyo imetokea wilayani Kwimba, Mkoa wa Mwanza, ambako habari zinadai watu hao maskini wanatishiwa kushtakiwa iwapo hawatalipa fedha na kupewa vitambulisho hivyo vya rais. Uchunguzi wa gazeti ...

Read More »

Mhasibu Wizara ya Afya kizimbani

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imemfikisha mahakamani Mhasibu wa Wizara ya Afya, Yahaya Athuman (39) akishitakiwa kwa makosa 20 yakiwamo ya kughushi nyaraka na kuisababishia serikali hasara ya  Sh milioni 34 zilizotolewa na serikali mwaka 2014 kwa ajili ya warsha kuhusu chanjo ya Rubela. Mhasibu huyo alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, mbele ya Hakimu Pamela ...

Read More »

Ushauri huu uzingatiwe

Wiki iliyopita wadau mbalimbali nchini pamoja na wengine kutoka jumuiya ya kimataifa walishiriki mdahalo mahususi kuhusu masuala ya biashara nchini. Katika mdahalo huo mengi yalijitokeza yenye lengo la kuboresha ili hatimaye kupata tija zaidi kwa upande wa tasnia ya biashara nchini. Itakumbukwa kuwa wiki kadhaa kabla ya mdahalo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, alifanya ...

Read More »

NINA NDOTO (23)

Itumie intaneti isikutumie   Kama kuna watu waliishi kuanzia miaka ya 1990 na kurudi nyuma ukiwarudisha leo duniani wataona maajabu mengi. Dunia imebadilika sana, imekuwa kama kijiji. Leo hii unaweza kuwasiliana na mtu aliyeko nje ya nchi kana kwamba ni jirani yako nyumba ya pili. Leo hii jambo lolote likitokea duniani ndani ya muda mfupi utakuwa umepata taarifa. Ama kweli ...

Read More »

Tumejipanga kuvihudumia viwanda

Wakati nchi ikijiandaa kwenda kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na baadaye Uchaguzi Mkuu 2020, Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) inazidi kuwapatia wananchi wa Dar es Salaam na Pwani maji. Ni wakati mwafaka kuwahamasisha na kuwaelimisha wananchi, viongozi wa serikali za mitaa pamoja na kamati za maji kuhusu namna bora ya usimamizi wa shughuli za maji ...

Read More »

Jinsi ya kuanzisha biashara Tanzania (19)

Wiki iliyopita nilihitimisha makala hii kwa kuainisha mapato yatokanayo na ajira ambayo kisheria unapaswa kuyalipia kodi kama mwajiriwa. Ni wajibu wa mwajiri kukata kodi hiyo ya zuio kwa pato la mwajiriwa pale anapompatia malipo hayo kila mwezi. Sitanii, jambo moja nilisisitize hapa, biashara nyingi zinapata tabu sana kutokana na kutofanya marejesho ya kodi kila miezi sita na kila baada ya ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (34)

Wameniteta naye huwa amewateta Kusemwa ni mtihani. Wameniteta naye huwa amewateta (Methali ya Wanyankole). Unanisengenya, wanakusengenya (Methali ya Wahaya). Wawili husengenya mmoja (Methali ya Wahaya). Huwezi kuwazuia ndege wasiruke juu ya kichwa chako, wataruka tu, lakini wakitaka kujenga viota lazima uje juu. Ni afadhali kuchoma mdomo kwa chakula kuliko kwa maneno. Kuwasema wengine vibaya au kusemwa vibaya ni jambo baya. ...

Read More »

Vigogo wa Serikali walaza nje familia ya watu 13

Kutoa maoni au uamuzi kuhusu jambo ambalo bado halijatolewa hukumu mahakamani ni kuingilia uhuru wa mahakama, hivyo unaweza kusababisha kupotosha mwenendo wa shauri au kesi iliyopo mahakamani. Jambo hilo linaweza kutendwa na mtu yeyote kwa kuzingatia masilahi anayopata kutoka upande mmoja anaoupigania au kwa kutokujua sheria inatoa tafsiri gani juu ya shauri lililopo mahakamani, ingawa kisheria jambo la kimahakama lazima ...

Read More »

Ndugu Rais ‘meseji’ ya Tshisekedi imefika?

Ndugu Rais safari yangu ya kwanza kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC ilinifanya niwaamini waliosema, tenda wema nenda zako, usingoje shukrani. Ujio wa Rais wa DRC ndugu Félix Tshisekedi umenikumbusha yaliyonitokea huko baada ya Rais Laurent Kabila kuikomboa Zaire kutoka kwa Mobutu Sesseseko. Kazad Nyembwe maarufu kama Didy au Mtoto wa Bwana aliniambia, “Mayega njoo Zaire upate kuelewa power ...

Read More »

Hatua rahisi za kutoa gari bandarini

Katika mfululizo wa makala za bandari, leo tunakuletea utaratibu unaotumika katika kuhudumia shehena ya magari hatua kwa hatua katika bandari za TPA, kuanzia meli inavyoingia bandarini, gari linavyoteremshwa kutoka melini, gari linavyopokelewa bandarini, gari linavyotoka bandarini hadi mteja kukabidhiwa gari lake. Ukaguzi baada ya meli kuwasili bandarini Hatua ya kwanza inayofanyika baada ya meli kuwasili bandarini ni ukaguzi unaofanywa na idara ...

Read More »

Ya AFCON, Taifa Stars na maagizo ya Rais Yoweri Museveni

Ukitaka kufahamu habari za mjini – mji wowote – muulize dereva wa teksi. Kwa kawaida ana taarifa nyingi na muhimu, na si ajabu kuwa hivyo. Anabeba abiria kila wakati na abiria kama ilivyo tabia ya binadamu yeyote, wana mdomo na hushindwa kukaa kimya kwa muda mrefu. Lazima watakuwa na kitu wanakiwaza na mawazo yanapozidi huyamwaga. Bila kuulizwa abiria watasema wanatoka ...

Read More »

Kuzuia mwanandoa kuuza ardhi ya familia

Kuna wakati katika maisha ya ndoa, mmoja wa wanandoa anaweza akataka kuuza au kubadili jina la nyumba ama  kiwanja bila ridhaa ya mwenzake ilhali nyumba hiyo ni ya familia. Lakini pia nje ya hilo kuna mazingira ambayo mtu anaweza kuwa si mwanandoa lakini mwenye masilahi katika nyumba au  kiwanja cha mtu fulani na anataka kuzuia nyumba ama kiwanja hicho kisibadilishwe ...

Read More »

Uponyaji wa majeraha katika maisha

“Nina uwezo mkubwa mno wa kuyafanya maisha yawe ya uchungu au ya furaha. Nina uwezo wa kuwa chombo cha maumivu makali au chombo cha kuvutia, naweza kunyanyasa au kutia hamasa, kuumiza au kuponya. Kama tukiwatendea watu  kadiri walivyo, tunawafanya wanakuwa wabaya zaidi. Kama tukiwatendea watu kama wanavyopaswa wawe tunawasaidia kuwa namna wanavyoweza kuwa.” Wolfgang Von Goethe. Kila mmoja wetu ameitwa ...

Read More »

Unabii wa kaka Rostam na mzee Kilomoni

Kutofautiana kimtazamo na mtu ambaye amekuwa mwajiri, kaka na rafiki yako, ni jambo linalohitaji roho ngumu. Lakini kwa kuwa tuko kwenye uwanja wa watani wa jadi, naomba leo nitofautiane kidogo na kaka yangu Rostam Aziz. Kabla ya kufanya hivyo, nitangaze masilahi mapema kwamba mimi ni mpenzi mtiifu wa Klabu ya Simba. Komredi Rostam ametamka bayana kuwa yeye ni Yanga kindakindaki. ...

Read More »

Waziri Mkuu, Butiama inahujumiwa

Mheshimiwa Waziri Mkuu, naandika barua hii mahususi kwako kuhusu Kijiji cha Butiama ambako ndiko Makao Makuu ya Wilaya ya Butiama. Uamuzi wa kuifanya Butiama kuwa Makao Makuu ya Wilaya ya Butiama ni utekelezaji wa uamuzi wa kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM kilichoketi hapa kijijini mwaka 2008 chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa wakati huo, Rais Jakaya Kikwete. Uamuzi ...

Read More »

Demokrasia na haki za binadamu – (3)

Wazungu walipoasisi demokrasia wakaweka na misingi mitatu ya kanuni za demokrasia ambazo ni uhuru wa majadiliano, uhuru wa walio wengi kufikia uamuzi na uhuru wa utii wa uamuzi uliokubaliwa katika kikao. Kadhalika walipotoa tangazo la haki za binadamu wakaweka vifungu vipatavyo thelathini vinavyoweka wazi haki za binadamu. Mathalani, haki ya kuishi katika uhuru, haki ya kulindwa na sheria, haki ya ...

Read More »

Yah: Ulinzi shirikishi ni laana?

Kuna wakati huwa naamini hakuna sababu ya kupeana salamu kutokana na matukio yanayotokea, kwa kawaida salamu anapewa mtu muungwana na anayepokea ni muungwana, lakini sasa hivi unaweza kutoa salamu ndiyo ukawa mwanzo wa kukaribisha nyoka katika mwili wako, kwa maana ya adui kukujua na kutekeleza adhima yake ya ubaya. Ninazidi kusikitika jinsi ambavyo hali inazidi kuwa mbaya kiusalama katika kipindi ...

Read More »

Gamboshi: Mwisho wa dunia (3)

Wiki iliyopita hadithi hii iliishia katika aya inayosema: “Mwanzoni nilimwona akiwa na urefu wa kawaida, lakini kadiri tulivyokaribiana alizidi kurefuka. Alikuwa anaongezeka mita moja kila hatua aliyopiga. Na baadaye nyayo za miguu yake zikawa zimeziba barabara kwa ukubwa wake,  nikaogopa asije akanikanyaga! Huwi! Huwi! Huwi!” Je, unafahamu nini kinafuata? Endelea… Nikaanza kupiga kelele katika kuzimia/kufa. Mara nikaona jamaa zangu wakinishikilia kwa nguvu ...

Read More »

Viungo Stars mhh…

Taifa Stars imeanza vibaya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa kukubali kipigo cha magoli 2-0 dhidi ya Senegal (Simba wa Teranga) katika dimba la Juni 30, jijini Cairo, Misri. Goli la kwanza la Senegal lilifungwa na Keita Balde katika dakika ya 28 ya kipindi cha kwanza. Bao hilo lilidumu hadi kipindi cha pili baada ya Diatta kufunga ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons