Author Archives: Jamhuri

Maisha bila maadui hayana maana (2)

Kutokusamehe kunaweza kukuangamiza wewe binafsi; kucheua ubaya uliotendewa, kulea uchungu, ni kudonoa kwenye donda lililo wazi na kukataa kuliruhusu lipone. Kuendelea kwetu kucheua kukwazika, kubaki kwetu katika uchungu nafsini mwetu, mawazo yaliyojaa chuki, kutaka kwetu kulipa kisasi, hakumuumizi kabisa mtu mwingine aliyetutesa na hakutuletei sisi jema lolote zaidi ya kutufanya sisi tuharibikiwe milele. Mawazo haya hufanya nafsi zetu zinywee (hivyo ...

Read More »

Haya ya Arusha yako nchi nzima

Nianze kwa kumpongeza Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk. Maulid Madeni, kwa kusaidia umma kutambua ukweli wa kile nilichokiandika kwenye safu hii toleo lililopita. Dk. Madeni amezuru maeneo mbalimbali ya jiji hilo na kubaini wafanyabiashara zaidi ya 500 walioamua kuwatumia wamachinga kuuza bidhaa zao, huku [wafanyabiashara] wakidai wamefunga biashara kwa kukosa wanunuzi. Kwa maelezo yake, amebaini udanganyifu mkubwa kwa wafanyabiashara ...

Read More »

Mikiki ya Chuo Kikuu Huria

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Profesa Elifas Bisanda, amezungumza na Gazeti la JAMHURI kuhusu historia, mafanikio, changamoto na hatima ya chuo hicho. Mwandishi MANYERERE JACKTON, aliyezungumza naye, analeta maelezo ya Profesa Bisanda neno kwa neno. Endelea…   Uhaba wa fedha Basically wanafunzi tunao, unaona operesheni yetu ni kubwa sana. Vituo 30 si kwamba tuna majengo – tunapanga, ...

Read More »

Valencia alia na Mourinho

Nahodha wa Klabu ya Manchester United, Antonio Valencia (33), amesema Meneja wake, Jose Mourinho, amemnyang’anya kitambaa cha unahodha bila sababu ya msingi. Amesema Mourinho alisingizia kwamba yeye ni majeruhi, jambo ambalo si kweli, huku akisema huo ulikuwa ni uamuzi binafsi wa kocha wake. Amesisitiza kwamba hana jeraha lolote, bali huo ni uamuzi wake binafsi. Kwani hana jeraha lolote. Hivi karibuni Kocha wa ...

Read More »

Trouble-Free Programs Of Mail-Order Brides reviews Revealed

Ways to Seduce Gals – Trying a Female’s Sexuality As a spiritual counselor, I acquire many cell phone calls from people who find themselves getting excited about someone to grown to be his or her’s ideal absolutely adore partner, soul mates as well as twin flame. I here’s always asked the moment this man can show all the way up ...

Read More »

Benki ilivyomwibia mteja kwa usanii

Baada ya Gazeti la JAMHURI kuchapisha habari ya kwanza kwenye toleo Na. 371 ikionyesha jinsi Benki ya BOA inavyoibia wateja nchini kwa maofisa wake kughushi nyaraka za wateja na kujipatia mikopo, sasa yameibuka mambo ya kutisha, JAMHURI linaripoti. Wamejitokeza wateja zaidi ya 50 wanaolalamika kuibiwa na maofisa wa BOA kwa nyakati tofauti, kwa utaratibu ule ule wa nyaraka zao kughushiwa ...

Read More »

Barua ya wazi kwa Rais wa Tanzania

Je, GMOs ni Sera ya Serikali? Mheshimiwa Rais; Kwa heshima na taadhima, niruhusu mimi mtoto wa mkulima mdogo na mwananchi wa nchi yetu tukufu nikusalimu. Hali yangu mimi na wanafamilia wenzangu, ambao ni wakulima wadogo nchini, si njema kabisa. Mheshimiwa Rais, kama ujuavyo, sisi ni takribani asilimia zaidi ya 70 ya wananchi wote, na naamini kuna ndugu zako wa damu ...

Read More »

Magufuli avunja rekodi

Rais John Magufuli katika kipindi chake cha uongozi cha miaka mitatu amefanya mengi ambayo hata wakosoaji wake wanakiri kuwa ni ya kupigiwa mfano. Kwenye toleo hili maalumu, tumeorodhesha baadhi ya mambo hayo yakilenga kuonyesha mafanikio makubwa katika kuimarisha nidhamu, uadilifu na uwajibikaji ndani ya utumishi wa umma na kukemea uzembe na kujenga ari ya kufanya kazi. Amefanikisha ununuzi wa meli ...

Read More »

Waenda Uingereza kuchangisha fedha za ‘mapambano’ Loliondo

Mgogoro wa masilahi katika Pori Tengefu la Loliondo (LGCA) unafukuta upya baada ya Watanzania takriban 20 kutarajiwa kusafiri kwenda nchini Uingereza wiki hii kuomba fedha za kuendeshea mapambano dhidi ya serikali. Uchunguzi uliofanywa na JAMHURI umebaini kuwa harambee ya kukusanya fedha hizo imeandaliwa na asasi ya The Oakland Institute ya nchini Marekani. Fedha zinazotarajiwa kukusanywa, pamoja na mambo mengine, zinalenga ...

Read More »

Mwenyekiti Baraza la Ardhi akataliwa

Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya ya Moshi, James Silas, amekataliwa kuendelea kusikiliza shauri la ardhi namba 175/2017 lililopo mbele yake. Oktoba 6, mwaka huu, Donald Kimambo na David Kimambo waliandika barua wakimtaka Silas kujitoa kusikiliza shauri lao. Barua hiyo imeeleza kuwa wamechukua uamuzi huo baada ya Silas kufuta shauri lao bila kusikiliza pande zote, hivyo kutotenda haki.  ...

Read More »

Hongera Rais Magufuli

Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli imetimiza miaka mitatu tangu ilipoingia madarakani mwaka 2015. Rais Magufuli alishika uongozi nchi ikiwa inakabiliwa na matatizo mengi ya kiuchumi, kijamii na kimaadili. Hatuna kipimo sahihi cha kubainisha kazi zilizokwisha kufanywa na Serikali ya Awamu ya Tano kwa miaka hii mitatu, lakini itoshe tu kusema yapo mambo mengi; makubwa, mazuri ...

Read More »

Jifunze kufikiri

Kuna wakati utahitaji kutumia akili za ziada zaidi ya kutumia akili za darasani. Ni watu wachache mno ambao wana uwezo huo. Tunaweza kusema watu hawa ni watu “waliojiongeza” kiakili. Watu wa namna hii ni watu wanaofikiri. “Palipo na mafanikio: Watu hawapimwi kwa urefu au ufupi, shahada za chuo au familia walizotoka, wanapimwa kwa uwezo wao wa kufikiri,” alisema David Schwartz. Naye ...

Read More »

USAID, JET wafunda wanahabari

“Watanzania hawajitangazi, wao wamekazana kutangaza wanyamapori na vivutio vya utalii peke yake, kama hatujitangazi kwanza sisi wenyewe, hawa wanyamapori mnafikiri wanatutangaza vyakutosha huko duniani?” Ni Maneno ya Dk. Ellen Oturu, Mratibu wa Miradi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), katika semina ya mafunzo ya wanahabari kuhusu uhifadhi wa mazingira, wanyamapori na utalii hapa nchini. Mafunzo hayo ...

Read More »

Raila Odinga anakuwa Rais Kenya (6)

Wiki iliyopita makala hii iliishia kwa kusema wawili hao (Ruto na Waigui) wanahaha kusafisha majina yao, huku Rais Kenyatta akiwa kimya. Jambo jingine linalomtia tumbo joto (Ruto) ni kitendo cha Odinga kujipenyeza kwenye Mkoa wa Bonde la Ufa, ambao ni ngome kubwa ya Ruto anayeungwa mkono na kabila lake la Wakalenjini. Endelea… Odinga kwa sasa amejenga uswahiba na Seneta wa Baringo, ...

Read More »

Tumejipanga kuvuka nje ya mipaka

Mwezi huu, Novemba 5, 2018 Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli ilitimiza miaka mitatu madarakani. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Sam Kamanga, amesema Rais Magufuli amesaidia kufufua shirika hilo. Katika mahojiano na JAMHURI, Kamanga ameeleza kuwa Rais Magufuli amesaidia Watanzania wamekuwa wazalendo, hivyo kuweza kuongeza wateja wa shirika. Kamanga anasema kwamba rais amesaidia ...

Read More »

Ngorongoro: Haijapata kutokea

MAELEZO YA MHIFADHI MKUU NCAA,  DK. FREDY MANONGI Ngorongoro ya miaka mitatu Ukiangalia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na eneo lenyewe kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita, mabadiliko yaliyoonekana ni makubwa kuliko kipindi chote eneo hili lilipoanzishwa mwaka 1959. Mabadiliko yametokea makubwa sana. Nianze upande wa mapato: Mapato kabla ya mwaka 2015 yalikuwa yamekwama kwenye takriban Sh bilioni 60 kwa ...

Read More »

Rais Magufuli ameimarisha Bandari – Kakoko (2)

Wiki iliyopita makala hii iliishia katika eneo ambalo Mkurugenzi Mkuu, Injinia Deusdedith Kakoko, alisema kila mkurugenzi na meneja wa ngazi yoyote anayefanya kazi Bandari amepewa malengo ya kutimiza. Lengo kuu ni kukusanya Sh trilioni 1 katika mwaka huu wa fedha. Katika makala hii Injinia Kakoko anaelezea kuhusu hatima ya watendaji wazembe watakaoshindwa kufikia malengo. Endelea… Wakati tukipunguza matumizi yasiyo ya ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (3)

Majaribu ni mtihani. Kumbuka kuwa bahari shwari haitoi wanamaji stadi. Watu wema wamefinyangwa na mitihani ya maisha yenye sura mbaya. Nakubaliana na Matshona aliyesema: “Roho zenye urembo zinafinyangwa na mapito yenye sura mbaya.” Wakati mwingine tunawajua watu wenye majina makubwa lakini hatujui majaribu makubwa waliyoyapitia. Tunajua umaarufu wao, hatujui hadithi zilizojaa huzuni za maisha magumu waliyoyapitia. Kila jambo zuri ambalo ...

Read More »

Maisha bila changamoto hayanogi (2)

Maisha bila maadui hayanogi. Maadui katika maisha ni kama viungo kwenye mboga, wanayanogesha maisha. Wanayapamba maisha ili yavutie, maadui wanakufanya umtafute na kumkumbuka Mungu usiku na mchana. Kama una maadui wewe ni wa kupongezwa na kama hauna maadui jitafakari upya. Kukosa maadui katika maisha ni kukosa changamoto muhimu za maisha. Watakatifu walioko mbinguni enzi za uhai wao hapa duniani walikuwa ...

Read More »

Namuomba Rais wetu atafakari ‘huruma’ aliyowapa wamachinga

Hakuna shaka kwamba Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais John Magufuli imefanya mambo mengi mazuri katika kipindi hiki cha miaka mitatu. Yapo pia mengine ambayo anakosolewa, na baadhi ya watu wanasema laiti kama angeyatenda kwa kadiri ya mtazamo wao, basi historia yake ingeandikwa kwa wino wa dhahabu kwenye kumbukumbu za uongozi wa taifa letu. Hili si ...

Read More »

Ahadi ni ukweli na maendeleo

Nitatumikia nchi yangu na watu wake wote. Nitajielimisha kwa kadiri ya uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote. Nitasema ukweli daima, fitina kwangu mwiko. Hizi ni ahadi tatu kati ya kumi za mwanachama wa TANU.  Ukizitazama kwa utulivu na ukazitafakari ahadi hizi utabaini zimebeba neno UKWELI na kuacha neno UONGO. Si kwa TANU tu chama cha siasa, ...

Read More »

Kampeni za Makonda na chenga ya Dk. Mahiga

Kampeni ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, za kusaka watu ambao wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja imeibua mjadala mkali wa sheria, tabia, na tafsiri ya vyote viwili. Sheria iko wazi: Ni kosa la jinai kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja. Lakini si kosa nchini Tanzania pekee. Taarifa ya mwaka 2016 ilibainisha zipo nchi 74 zenye ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons