Sitanii

MV Nyerere imeamsha uchungu

MV Nyerere imeamsha uchungu Na Deodatus Balile Ajali ya MV Nyerere iliyotokea Septemba 20, 2018 katika Ziwa Victoria imeamsha uchungu wa wakazi wa Kanda ya Ziwa. Imenikumbusha siku ya Jumanne ya Mei 21, mwaka 1996 ilipozama meli ya MV Bukoba na kuua watu zaidi ya 800. Takwimu zinatofautiana. Wapo wanaosema walikufa watu 1,000 na wengine wanasema walikufa 800. Vivyo hivyo ...

Read More »

Lissu ameumizwa, lisitokee tena Tanzania

Na Deodatus Balile Leo nimeona niandike mada inayohusiana na hali ya usalama, amani, utulivu na upendo kwa taifa letu. Nimesoma maandishi ya Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu, wakati anatimiza mwaka mmoja wa maumivu tangu alipopigwa risasi Septemba 7, 2017 jijini Dodoma. Si nia yangu kurejea aliyoyasema Lissu, ila kwa picha ya video niliyoiona, inayoonyesha kuwa mfupa wake wa ...

Read More »

Utawala wa sheria utatuepusha ya Makonda

Na Deodatus Balile Wiki tuliyoimaliza imekuwa na matukio mengi. Tumesikia kifo cha Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa Hospitali ya Rufaa Bugando, Mtawa Susan Bathlomeo. Kifo hiki kimeacha maswali mengi. Wapo wanaosema amejirusha, wapo wanaosema amerushwa kutoka ghorofani. Mpaka sasa uchunguzi unaendelea na hatujapata jibu kamili. Sitanii, mwezi Agosti umekuwa na vifo vingi kwa kiwango cha kutisha. Wakati tunaomboleza kifo ...

Read More »

Tamu, chungu ya Magufuli

Na Deodatus Balile Leo zimepita wiki mbili bila kuandika katika safu hii. Makala yangu ya mwisho niliahidi kuandika yaliyojiri katika safari ya mwisho niliyokwenda Mwiruruma, Bunda kumzika Comrade Shadrack Sagati (Mungu ailaze mahala pema peponi roho yake). Sentensi ya mwisho katika makala yangu ilisema: “Olwo mumywanyi wawe kufa afelwa.” Hii ina maana, kuliko rafiki yako kufariki dunia, ni bora afiwe. ...

Read More »

Waziri Lugola maliza sakata la Lugumi

Ni miaka miwili na nusu sasa tangu Watanzania walipoanza kusikia kuhusu sakata la Kampuni ya Lugumi Enterprises kushindwa kufunga vifaa vya kuchukulia alama za vidole kwenye vituo 108 vya Polisi, kama mkataba wa kampuni hiyo na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ulivyotaka. Jambo hilo liliibuliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Juma Assad, ...

Read More »

Rais Magufuli fungua milango zaidi

Na Deodatus Balile   Wiki iliyopita Rais John Pombe Magufuli amefungua milango ya kukutana na viongozi wastaafu. Amekutana nao Ikulu na akasema utaratibu huu ataundeleza. Akasema atakutana nao mara kwa mara na katika kukutana nao hakuwabagua. Amekutana na wale walioko Chama Cha Mapinduzi (CCM) na hata wale waliohamia upinzani kama Edward Lowassa na Frederick Sumaye. Sitanii safu hii ni fupi. ...

Read More »

Bomu la watu laja Afrika – 4

Balile

Wiki tatu zilizotangulia kabla ya wiki iliyopita, nilichambua kitabu kinachohusu njia mbadala za kufufua uchumi wa Afrika. Nilikisitisha wiki iliyopita tu, kutoa fursa ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani. Kitabu hiki kinaitwa “Making Africa Work”. Tafsiri isiyo rasmi ya jina la kitabu hiki inamanisha “Mbinu za Afrika Kujikwamua Kiuchumi.” Kitabu hiki kimeandikwa na Greg Mills, Olusegun Obasanjo ...

Read More »

Uhuru wa habari uanzie kwenye vyumba vya habari

DODOMA. EDITHA MAJURA. Serikali na Vyombo vya habari, wametuhumiana kuminya uhuru wa vyombo vya habari nchini. Wakati serikali ikituhumiwa kutofanya vizuri katika kudhibiti usalama wa wanahabari wanapotekeleza majukumu yao, serikali nayo imesema vyombo vya habari vinaminya maslahi ya wanahabari kiasi cha kusababisha washindwe kutekeleza majukumu yao kwa weledi unaohitajika. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, akijibu ...

Read More »

Bomu la watu laja Afrika – 3

Balile

Na Deodatus Balile Kwa wiki ya tatu sasa nafanya mapitio ya kitabu kiitwacho “Making Africa Work”. Tafsiri isiyo rasmi jina la kitabu hiki linamanisha “Mbinu za Afrika kujikwamua kiuchumi.” Kitabu hiki kimeandikwa na Greg Mills, Olusegun Obasanjo (Rais mstaafu wa Nigeria), Jeffrey Herbst na Dickie Davis. Kimechapishwa na Taasisi ya Brenthurst Foundation ya Johannesburg, Afrika Kusini. Rais (mstaafu) Benjamin Mkapa ...

Read More »

Bomu la watu laja Afrika -2

Balile

Na Deodatus Balile Wiki iliyopita nilizungumzia wingi wa watu unaokuja duniani na hasa Bara la Afrika. Tanzania kwa sasa inakadiriwa kuwa na watu milioni 58. Mwaka 1950 nchi yetu itakuwa na watu milioni 138. Afika kwa sasa inatajwa kuwa na watu bilioni 1.2 na mwaka 2050 itakuwa na watu bilioni 2.5, huku mwaka 2100 ikiwa na watu bilioni 5.7 sawa ...

Read More »

Bomu la watu laja Afrika

Balile

Na Deodatus Balile Mpendwa msomaji salaam. Wiki iliyopita sikuwa katika safu hii. Nilisafiri kwenda Kisarawe kidogo kwa ajili ya kupeleka taarifa za kilimo cha muhogo. Niliitwa na viongozi wa wananchi wa Kijiji cha Gwata, wilayani Kisarawe waliotaka kufahamu taratibu na jinsi ya kupata fursa ya kilimo cha muhogo nchini. Taratibu zinaendelea na nimewajulisha viongozi wa Gwata na kupitia safu hii ...

Read More »

Ujenzi wa viwanda, muhogo Na Deodatus Balile

Wiki iliyopita niliahidi kuanza kuandika masuala ya msingi katika kilimo cha muhogo. Nimepata simu nyingi kutoka kwa watu mbalimbali wakisema wanataka kulima muhogo, wengine tayari wanao muhogo na wengine wana mashamba au wengine wanatafuta mashamba ya kulima muhogo. Wengine wamepata furaha, na wengine wamekata tamaa. Nimebaini kuna kiwango kikubwa cha watu kukosa uelewa katika suala la kilimo. Wakati nawaza suala ...

Read More »

Kuna dalili muhogo unalimika

Balile

Na Deodatus Balile, Beijing, China Naandika makala hii wakati naanza safari ya kurejea nyumbani baada ya kuwa hapa nchini China kwa muda wa wiki mbili hivi. Nimetembelea vyuo vikuu viwili, miji minane na maonyesho ya zana za kilimo. Ziara hii imefadhiliwa na Bill & Melinda Gates Foundation, Ubalozi wa Tanzania nchini China, Ubalozi wa China nchini Tanzania na Wakfu wa ...

Read More »

Mlango wa viwanda Tanzania upo China

Na Deodatus Balile, Beijing   Wiki iliyopita katika safu hii nimeeleza kuwa nimeanza kuandika makala zinazohusiana na viwanda. Nimesema nimeingalia familia ya Watanzania, nikaangalia ugumu wa kazi wanazofanya na aina ya kipato wanachoweka kibindoni, basi nikapata hamu ya kuhakikisha angalau nahamasisha Watanzania 1,000 wanamiliki viwanda. Naushukuru Ubalozi wa Tanzania nchini hapa, Ubalozi wa China nchini Tanzania na taasisi ya Bill ...

Read More »

Siasa zimetosha, tuingie viwandani

Na Deodatus Balile   Miaka ya 1950 wakati Tanganyika inapigania Uhuru lengo kuu lilikuwa ni kukomboa watu wetu kutokana na unyanyasaji wa hali ya juu waliokuwa wanafanyiwa na Wakoloni. Hali ilikuwa hivyo hivyo kwa upande wa Zanzibar dhidi ya Waarabu. Wakoloni hawa walikuwa wanatulimisha kwa faida yao binafsi. Watu wetu walilima pamba, korosho, karafuu, mbaazi, karanga, kahawa na mazao mengine ...

Read More »

Utumikishwaji: Bomu linalowalipukia watoto Dodoma

Na Zulfa Mfinanga, Dodoma Vitendo vya utumikishwaji wa watoto bado vinaendelea nchini licha ya kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi 193 zilizokubaliana juu ya ukomeshaji wa ajira kwao. Tanzania ni miongoni mwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa (UN) waliosaini azimio la kulinda haki za mtoto maarufu kama UN Convention on the Rights of the Child lililopitishwa mwaka 1990. Mkutano ...

Read More »

Akwilina awe Balozi wa amani

Ijumaa ya Februari 16, mwaka 2017 imekuwa siku ya majonzi kwa taifa letu. Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwiilina B. Akwilini ameuawa kwa kupigwa risasi akiwa kwenye daladala, wakati polisi wanapambana na waandamanaji wa Chadema. Wiki iliyopita nimeandika makala nikitahadharisha juu ya mwenendo wa askari polisi kutumia nguvu kubwa katika masuala ya uchaguzi. ...

Read More »

Uchaguzi Tanzania tutavuna tunachopanda

Balile

Kwa siku za karibuni nimejipa jukumu la kusoma vitabu vitakafitu. Nasoma Biblia na Korani Tukufu. Nasoma maandiko matakatifu. Katika safu hii sitarejea Biblia wala Korani Tukufu, bali ujumbe mmoja tu kutoka vitabu hivi – MAONYO YA MAKUHANI na wengine wanaoitwa manabii kwa njia ya nyaraka. Kila walichokiona walikiandika. Ndiyo maana leo tunasoma Biblia au Korani Tukufu na kupata historia na ...

Read More »

CCM, CHADEMA Jiandaeni Kisaokolojia

Wiki hii unafanyika uchaguzi mdogo katika majimbo ya Kinondoni, Dar es Salaam na Siha, Kilimanjaro. Uchaguzi huu umeitishwa kutokana na waliokuwa wabunge Godwin Mollel (CHADEMA) na Maulid Mtulia (CUF) kuhama vyama vyao wakajiunga na CCM baada ya kuvutiwa na utendaji wa Rais John Magufuli. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewateua Mollel kuwa mgombea wake Siha na Mtulia kuwa mgombea wake Kinondoni. ...

Read More »

Siku Afrika ikiwa kama Marekani itakuwaje?

Na Deodatus Balile   Kwa muda sasa nafuatilia siasa za Afrika na sehemu nyngine duniani. Leo nitajadili mataifa mawili; Marekani na Kenya. Nafuatilia kinachoendelea nchini Marekani. Nafuatilia kinachoendelea nchini Kenya. Narejea misingi ya uhuru wa mawazo na uhuru wa vyombo vya habari. Nchini Marekani tangu umalizike uchaguzi mkuu wa Novemba, 2016, Rais aliyeshinda, Donald Trump amekuwa kwenye chetezo. Kutokana na ...

Read More »

NDUGU RAIS NAKUPONGEZA HATA KAMA HAWAPENDI

Ndugu Rais, nakupongeza kwa kuwaumbua akina ‘Grace’ wetu wanaokupigia chapuo uongezewe miaka ya urais. Wangekuwa ni watu wa kuona aibu wangetafuta mahali pa kuzificha sura zao. Lakini wauza utu sawa na wauza miili. Aibu waipate wapi? Kama Mugabe angempuuza Grace wake kama ulivyowapuuza hawa ‘Grace’ wetu, nina hakika Robert Mugabe angekuwa bado ni Rais wa Zimbabwe. Siyo kwamba wana mapenzi ...

Read More »

Mbowe Kususa Uchaguzi Unaua Upinzani

Kwa mara nyingine ndugu msomaji naomba kukupa heri ya mwaka mpya 2018. Najua utakuwa umeshangaa leo inakuwaje naandika juu ya uchaguzi na naacha kugusia suala la muhogo. Muhogo sitauacha. Chini ya makala hii naeleza fursa mpya iliyopatikana ya muhogo. Kelele nilizopiga zimeanza kuzaa matunda. Mungu anaipenda Tanzania na nitaeleza kwa kina kwa nini napigania muhogo. Mwishoni mwa wiki Kamati Kuu ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons