Maoni ya Mhariri

Busara itumike TRAWU

Wiki iliyopita Gazeti hili la JAMHURI lilichapisha habari kuhusu kashfa iliyojitokeza wakati wa maadhimisho ya kilele cha Siku ya Wafanyakazi, Mei Mosi, kwa mwaka huu yaliyofanyika kitaifa jijini Mbeya. Kashfa hiyo imekikumba Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU). Ndani ya chama hicho, baadhi ya viongozi wake wanadaiwa kuwasilisha jina la kigogo asiyestahili kuwa mfanyakazi bora ili apewe mkono na ...

Read More »

Haki itendeke katika hili

Moja ya habari zilizochapishwa na gazeti hili ni kuhusu kupotea katika mazingira ya kutatanisha kwa mtuhumiwa wa uhalifu, Josephat Jerome Hans, akiwa mikononi mwa Jeshi la Polisi mkoani Dodoma. Habari hiyo imeeleza kuwa kijana huyo anatuhumiwa kwa wizi wa Laptop katika moja ya nyumba za kulala wageni Dodoma. Tayari mama mzazi wa mtuhumiwa huyo, Lusina Joseph Kiria, ameandika malalamiko yake ...

Read More »

Mchango wa CAG Mei Mosi hii utambuliwe

Mei Mosi mwaka huu wafanyakazi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaungana na wafanyakazi wenzao kwingine duniani kuadhimisha siku ya wafanyakazi. Kwa kawaida mataifa karibu yote duniani huadhimisha siku hii kwa namna tofauti, lakini yenye baadhi ya matukio yanayoshabihiana kama maandamano ya makundi ya wafanyakazi wa sekta tofauti wakiwa na mabango yenye ujumbe wanaoulenga kwa sababu mahususi kwa mujibu wa ...

Read More »

Bodi ya Ngorongoro isifumbiwe macho

Miongoni mwa habari tulizozipa umuhimu wa juu hivi karibuni ni ile inayohusu matumizi mabaya ya fedha yanayofanywa na Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlala ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA). Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amebaini kuwa kwa mwaka uliopita, bodi hiyo iliketi vikao 20 badala ya vikao vinne vya lazima na viwili vya kazi za ukaguzi na ...

Read More »

Kauli ya Dk. Bashiru ni mwanga kwa nchi yetu

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, amezungumza maneno mazito ambayo kwa yeyote anayeitakia heri nchi yetu yamemgusa. Maneno aliyoyasema yanaweza yasiwafurahishe wengi, hasa ndani ya chama chake, lakini huo ndio ukweli wenyewe. Ameonya juu ya mmomonyoko wa haki miongoni mwa wananchi na vyombo vya utoaji haki, na kuonya kuwa mataifa kama Sudan ambayo utawala wake umeangushwa ...

Read More »

Wanaolalamikiwa warejee hotuba ya Rais bungeni

Novemba 25, mwaka 2015, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, alifungua Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kulihutubia. Katika hotuba yake hiyo, Rais Magufuli alibainisha mambo kadhaa aliyokuwa ameyabaini wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 moja kwa moja kutoka kwa wananchi. Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na suala la rushwa. Akasema ...

Read More »

Msajili wa Vyama awe mlezi wa vyama

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imetoa tishio la kukifuta Chama cha ACT-Wazalendo. Sababu kadhaa zimetolewa, zikiwamo za madai kwamba chama hicho kinatumia udini na kinaharibu kadi na mali za chama kingine – CUF. Tunaandika haya kwa unyenyekevu mkubwa tukitambua kuwa dola na vyombo vyake vina dhima ya kuhakikisha nchi yetu inaendelea kuwa tulivu na salama. Kwa kulitambua hilo, ...

Read More »

Utulivu uendelee vyama vya siasa

Katika siku za karibuni uwanja wa siasa nchini umeshuhudia matukio makubwa. Ni matukio yenye kuzua mjadala na kimsingi, unaweza kusema ni matukio ambayo kwa sehemu kubwa yamevuruga mikakati ya vyama vya siasa kwa ujumla wake, mikakati kati ya chama kimoja dhidi ya kingine na hata mikakati kati ya mwanasiasa mmoja hadi mwingine. Matukio haya yanahusu baadhi ya wanasiasa wenye majina ...

Read More »

Namna ya kukomesha ubambikaji kesi Polisi

Wiki iliyopita katika hali isiyokuwa ya kawaida kwa miaka mingi, Jeshi la Polisi Tanzania limekuwa miongoni mwa taasisi za kitaifa zilizothibitisha kuwa chombo hicho kimewahi kuhusika kubambikia baadhi ya wananchi kesi. Baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kudai kuwa Jeshi la Polisi kupitia kwa baadhi ya askari wake walimbambikia kesi mmoja wa wafanyabiashara mkoani Tabora, Jeshi la Polisi kupitia kwa ...

Read More »

Tanzania tunao wajibu wa kuziokoa Rwanda, Uganda

Fukuto la kutokea mfarakano na hata umwagaji damu linaendelea kati ya Uganda na Rwanda. Lakini pia kuna msuguano mkubwa wa kidiplomasia kati ya Rwanda na Burundi. Mataifa haya matatu ni wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hii ina maana kwamba jambo lolote baya katika mataifa hayo lina athari kwa nchi wanachama, hasa Tanzania. Tanzania ni mwathirika mkuu kwa sababu tunapakana ...

Read More »

Uamuzi wa Lowassa ni fursa kwa Dk. Magufuli 

Waziri Mkuu (mstaafu), Edward Lowassa, mwishoni mwa wiki iliyopita alifanya uamuzi mwingine mgumu katika maisha yake ya kisiasa.  Kama ilivyo kawaida yake katika kufanya uamuzi mgumu kwenye maisha yake ya uongozi nchini, Lowassa alirejea katika Chama chake cha awali, Chama Cha Mapinduzi (CCM), akitokea Chama kikuu cha upinzani – Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).  Uwepo wa Lowassa Chadema katika kipindi chake cha ...

Read More »

Tuongeze uwekezaji elimu

Kwa muda sasa tunapata taarifa kutoka sehemu mbalimbali za nchi juu ya uhaba wa vyumba vya madarasa kwa watoto walioshinda mtihani wa darasa la saba kwenda kidato cha kwanza mwaka 2018. Malalamiko ya ukosefu wa vyumba vya madarasa yameanza kujitokeza si tu katika ngazi ya sekondari, bali hata ngazi ya shule za msingi. Kwa mfano Shule ya Msingi Kyakailabwa, katika ...

Read More »

Matokeo utafiti wa habari yawe changamoto

Wiki iliyopita Taasisi ya utafiti ya Spurk Media Consulting Ltd ya Uswisi kwa kushirikiana na Baraza la Habari Tanzania (MCT), imetangaza matokeo ya utafiti wake uliohusu ubora wa maudhui kwa vyombo vya habari nchini kwa mwaka 2018. Matokeo ya utafiti huo kwa vigezo vya watafiti, vikalifanya Gazeti la JAMHURI kuongoza. Tunawashukuru wasomaji wetu pamoja na timu nzima ya wafanyakazi wa JAMHURI ...

Read More »

Mauaji Njombe hayakubaliki

Habari kubwa katika gazeti letu la leo inahusiana na mauaji ya watoto yanayoendelea mkoani Njombe. Serikali kupitia vyombo vya dola imeimarisha ulinzi na usalama Njombe. Bunge limeombwa kuunda kamati ya kuchunguza mauaji haya. Uchunguzi wa Gazeti hili la JAMHURI umebaini kuwa mauaji haya yanatokana na imani za kishirikina. Mmoja wa watu wanaoshikiliwa na vyombo vya dola atakayefikishwa mahakamani muda wowote ...

Read More »

Tusikubali TAZARA ifilisiwe

Habari iliyopewa uzito wa juu kwenye gazeti hili toleo la leo inahusu ‘kuuzwa’ kwa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA). Mengi yamebainishwa kwenye habari hiyo, lakini lililo kubwa ni mpango wa ‘ubinafsishaji’ wake kwa kampuni ya Afrika Kusini. Tunatambua kuwa Reli ya TAZARA au kwa jina jingine Reli ya Uhuru, imekuwa ikipitia vipindi vigumu vya uendeshwaji wake. Mara ...

Read More »

Kamwe tusijisahau, tuwe macho dhidi ya magaidi

Kwa mara nyingine genge la magaidi limeshambulia na kuua majirani zetu kadhaa wa jijini Nairobi, Kenya. Imeripotiwa watu 21 wamepoteza maisha kwenye shambulizi hilo. Tunawapa pole ndugu wa marehemu, majeruhi na wote walioathiriwa kwa namna moja au nyingine na tukio hilo. Kwa namna nyingine magaidi wamedhihirisha kuwa wapo na pia dunia si salama kama baadhi yetu wanavyodhani. Hizi ni salamu ...

Read More »

‘Manabii’ wa kangomba wasakwe, waadhibiwe

Mwangwi wa kilio cha wakulima wa korosho unazidi kusikika pande zote za nchi. Idadi kubwa ya wanafunzi wamekwama kwenda shuleni. Wale waliofaulu darasa la saba wameshindwa kuripoti shule za sekondari kwa ukosefu wa nguo na vifaa vya masomo. Hata wale ambao kwa kawaida hawapendi watoto wao waendelee na masomo ya sekondari wamepata kisingizio cha ukosefu wa fedha za korosho. Hali ...

Read More »

IGP inusuru Tunduru

Katika toleo la leo tumechapisha taarifa za magendo ya zao la korosho, maarufu kama ‘kangomba’ inayoendelea katika mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi. Kwa kiasi kikubwa, habari hiyo imejikita katika Mkoa wa Ruvuma, Wilaya ya Tunduru. Watendaji wa umma katika ngazi ya wilaya wametajwa kwa kiasi kikubwa kuhusika katika biashara ya kangomba. Askari PC Mtaki ametajwa kutoa fedha za kununulia ...

Read More »

Asanteni wasomaji wetu

Wiki iliyopita, yaani Desemba 6, 2018 Gazeti la JAMHURI limetimiza miaka saba sokoni. Sasa tumeanza mwaka wa nane. Katika kipindi chote hicho cha miaka saba hatujawahi kushindwa kwenda sokoni. Tumechapisha kwa ukamilifu matoleo yote 52 kila mwaka na ya ziada tulipopata matoleo maalumu. Ndiyo maana toleo la leo ni la 376. Katika maoni yetu ya Desemba 6, 2011 tulipotoa nakala ...

Read More »

Hii ni aibu rushwa kukwamisha stendi

Habari tuliyoipa umuhimu wa pekee kwenye toleo hili inahusu mkwamo wa ujenzi wa stendi ya kisasa ya mabasi ya mikoani eneo la Mbezi Luis, Dar es Salaam. Tumeeleza namna vitendo vya rushwa vinavyotishia mradi huo mkubwa kwenye sekta ya usafiri wa mabasi nchini na katika ukanda huu wa Afrika Mashariki. Ni jambo la bahati mbaya kuona kuwa bado tunao baadhi ...

Read More »

Hongera Wizara ya Kilimo, hongereni wapambanaji

Wizara ya Kilimo imezuia Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) iliyopo Makutupora, Dodoma kuendelea na utafiti wa mbegu za GMO. Uamuzi huo ni majibu kwa kilio cha wazalendo waliojitokeza kupaza sauti kuhoji uhalali wa chepuo linalopigwa ili kuruhusu mbegu hizo kuanza kutumika nchini. Wasomi, wakulima na watu wa kada mbalimbali wamejitokeza kueleza kisayansi madhara ya mbegu za GMO yakiwamo magonjwa ...

Read More »

Uonevu kwa wakulima ufikie tamati

Tunapongeza hatua iliyochukuliwa na serikali kwa wakulima wa korosho. Japo matokeo ya uamuzi huo hayajajulikana, lililo la msingi ni kuwa serikali imeonyesha kuwajali wananchi hao. Historia inaonyesha kuwa kwa miongo mingi wakulima wa mazao ya aina zote wamekuwa wakidhulumiwa licha ya matamko mengi ya kuwatia moyo. Ufisadi mkubwa umekuwapo kwenye sekta hii kiasi cha kuwafanya wakulima wengi waishi na hatimaye ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons