JAMHURI YA WAUNGWANA

Kikwete na uteuzi dakika za mwisho

Rais Jakaya Kikwete, wiki ijayo atakuwa ameingia kwenye orodha ya marais wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa kiongozi aliyechaguliwa mara mbili, na kufanikiwa kumaliza kipindi chake cha miaka 10 salama, si busara sana kuendelea kumjadili au kumkosoa. Watu waungwana wangependa kumwona kiongozi wetu anapumzika salama; na kwa maana hiyo ushauri wetu unapaswa kuelekeza kwa huyo anayekuja. Hata hivyo, ...

Read More »

Nilichekwa kwa kumnyenyekea Mwalimu Julius Nyerere

Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuishi karibu na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Nashukuru kwa sababu Watanzania wengi, na walimwengu kwa jumla waliitamani fursa hiyo, lakini hawakuipata moja kwa moja isipokuwa kupitia sauti na pengine maandishi yake. Mwalimu Nyerere anabaki kuwa mtu wa aina ya pekee ambaye si rahisi kumweleza. Nikiri kuwa sikuwahi kumzoea au kumfahamu. Kila nilipomkaribia, ...

Read More »

Tuwe tayari kuyakubali mabadiliko

Kadiri Uchaguzi Mkuu unavyokaribia, ndivyo joto lake linavyozidi kupanda miongoni mwa wafuasi wa vyama mbalimbali vya siasa. Watanzania wanataka mabadiliko. Ni kwa sababu hiyo, wagombea wakuu wa urais, Edward Lowassa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) anayewakilisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), anasikika akisisitiza mabadiliko. Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, anasisitiza mabadiliko, lakini akiongeza ...

Read More »

Mkicheka na wamachinga watatundika mitumba Ikulu

Kampeni za Uchaguzi Mkuu zinaendelea. Mengi yanazungumzwa na wagombea na wafuasi wao. Ahadi nyingi za wagombea urais zinalenga kuwashawishi wapigakura wawachague. Zipo ahadi zinazofanana. Elimu, maji, vita dhidi ya mafisadi na wala rushwa, mikopo kwa wajasiriamali, ajira na ukomeshaji aina zote za uonevu katika jamii, ni baadhi tu ya ahadi zinazowavutia wengi. Bila shaka kinachofanywa na wapigakura kwa sasa ni ...

Read More »

Kosa la Dk. Magufuli ni kusimamia sheria?

Nimesoma makala ya rafiki na kaka yangu Joster Mwangulumbi, iliyokuwa na kichwa cha habari: “Yako mengi tunayopaswa kuyatafakari”. Makala hiyo fupi, lakini kali, inamhusu mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli. Aya moja inasema: “Rais Kikwete na makanda wengine wanampamba Dk. Magufuli kwa sifa kwamba ni mzalendo, mwadilifu, mchapakazi na hana makuu, wanaficha ukweli kwamba Dk. Magufuli ...

Read More »

Wasiotii sheria wajifunze kuzitii kabla JPM hajaapishwa

Dk. John Magufuli, ameshaanza kampeni kwa ajili ya kuingia Ikulu ifikapo Oktoba, mwaka huu. Kwa kuwa ameshaanza kampeni, wengi wamesikia nini anachokusudia kuifanyia Tanzania na Watanzania. Hadi naandika makala hii, “mtani wa jadi” wa Dk. John Magufuli kwenye mchuano huu wa urais, Edward Lowassa, na Chadema kwa jumla walikuwa hawajaweka hadharani Ilani yao. Kwa sababu hiyo, nimeona nijadili hiki kilichokwishasikika ...

Read More »

CCM wa kweli wakiri hili

Wale wa rika langu, ama wamezaliwa, au wamelelewa na sasa wanaelekea kuzeeka ndani ya malezi yenye misingi iliyojengwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Watanzania wengi waliozaliwa kabla ya mwaka 1992 wanaijua CCM, na kwa kweli hawana namna ya kukwepa kuizungumza, kuijadili na wakati mwingine kuikosoa. Haishangazi kuwaona baadhi ya wanachama na viongozi walio nje ya chama hiki wakiguswa na nyimbo ...

Read More »

Naiona Serikali ya Mseto

Wale wanaopenda kutazama runinga wanaona kwa macho yao namna siasa za Tanzania zinavyobadilika kwa kasi kila siku. Mwishoni mwa wiki walionekana wananchi kwenye maeneo kadhaa katika vijiji vilivyopo mikoa ya Arusha na Tanga wakichoma na wengine wakichana kadi zao za uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kilichowashitua watazamaji wengi, si matendo ya kuchana au kuchoma kadi tu, bali ni aina ...

Read More »

Makongoro Nyerere: Nichagueni ninyooshe nchi

Mwaka huu ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu. Ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) tayari wamejitokeza watangaza nia 40 ambao wote wanawania kiti cha urais, waweze kumrithi Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu. Kila anayetangaza nia anayo maono ya nini anataka kuifanyia nchi hii kwa nia njema ya kututoa hapa tulipo tusonge mbele zaidi. Katika makala ...

Read More »

CCM ‘wasipogawana mbao’ nitashangaa!

Kiongozi wetu Mkuu anaendelea na ziara ya kuwaaga marafiki wetu wa maendeleo. Anazidi kuongeza idadi ya safari na siku alizokaa ughaibuni. Kwa Afrika, amejitahidi kuwaga kwa pamoja pale nchini Afrika Kusini. Lakini kwa Ulaya, Asia na Marekani, naona kaamua kwenda kuaga kila nchi kadri anavyoweza. Hii haishangazi kwa sababu kwa miaka 10 safari zake nyingi zimekuwa za Ulaya, Marekani na ...

Read More »

Tunamhitaji Rais Mtendaji Mahiri, Jasiri

Wanaowania urais wa Awamu ya Tano Tanzania, kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), walianza kuchukua fomu mjini Dodoma Jumatano Juni 3, 2015. Inaonekana wengine waliokuwa wanatajwatajwa, wanasita, hawajajitokeza kugombea, hawajachukua fomu! Labda watajitokeza baadaye, au wanaona hawana nafasi nzuri. Lakini jambo la kusikitisha ni ile hali ya kupakana matope iliyojitokeza wakati baadhi wagombea hao watarajiwa, walipokuwa wanatangaza nia. Badala ...

Read More »

Pinda angepumzika tu

Miaka kadhaa iliyopita, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, aliwaita wahariri wa vyombo vya habari ofisini kwake, Dar es Salaam. Akazungumza mambo mengi. Nilipata bahati ya kualikwa, na ya kumuuliza swali. Swali langu, ukiacha ule mgogoro alioshindwa kuutatua- mgogoro wa ardhi Kwembe-Kati, lilihusu ukwasi alionao. Akatoa maelezo marefu kwa kusema ana nyumba za kawaida- Pugu, Dar es Salaam na Kibaoni, Katavi. Kwenye ...

Read More »

CCM tunayoiona ni uhunzi wa Kikwete

Kuna ule msemo wa “vita ya panzi, furaha ya kunguru”. Vyama vya siasa vya upinzani, kama kweli vina dhamira ya dhati ya kupata uhalali kutoka kwa Watanzania, mwaka huu wa 2015 ni mwaka sahihi kabisa wa kutimiza azma hiyo. Endapo vyama hivyo, kupitia umoja wao wa Ukawa vitashindwa kutumia fursa hii, basi huenda Watanzania wakaendelea kushuhudia miaka mingine mingi ya ...

Read More »

Hatma ya Tanzania iko kwa Jaji Lubuva

Waliosoma maandishi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa zamani, Jaji Mark Bomani, watakubaliana na mawazo yake. Hoja yake kuu ni kwamba Katiba mpya katika mazingira ya sasa ya nchi yetu, haiwezekani. Kwa maana hiyo hatuwezi kuwa na Uchaguzi Mkuu mwaka huu kwa kutumia Katiba mpya. Jaji Bomani, mtu mzoefu wa shughuli za Serikali, anashauri Katiba ya sasa iendelee kutumika, lakini ...

Read More »

Yah: Sheria ya mitandao na vita ya utamaduni wa Mtanzania

Nimewahi mara kadhaa kuzungumzia juu ya utamaduni wa Mtanzania wa Tanzania, wakati huo nilikuwa sijawahi fikiria kama Serikali yetu ingeweza kuja na njia mbadala wa kutunga sheria ya kudhibiti matumizi ya mitandao ya simu na mifumo ya habari. Kwa kweli, nimefarijika sana na sheria hii hata kabla haijaanza kutumika, sheria ni kitu kingine na kutumika ni kitu kingine, uwepo wa ...

Read More »

Serikali makini haiwezi kusarenda

Nilipomuona Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudence Kabaka, akitengua uamuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) wa kuwataka madereva kurejea darasani, nilishangaa. Nilikuwa miongoni mwa tuliopigwa na bumbuwazi kwa uamuzi huo, ingawa walikuwapo mamia kwa maelfu walioshangilia. Uamuzi wa Serikali wa kukataa madereva kurejea darasani kusomea fani hiyo, umejidhihirisha sasa. Ndani ya miezi minne, wastani wa ...

Read More »

ACT kimbunga

Kumekuwapo mikutano ya siri inayowahusisha viongozi waandamizi wa Chama cha ACT-Wazalendo na baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao hawana hakika kama watatendewa haki wakati wa kupitishwa kwa majina ya wagombea urais. Mazungumzo hayo yamelenga kufungua njia kwa wana CCM hao kujiunga na chama cha ACT endapo watafanyiwa mizengwe ndani ya CCM. Habari kutoka kambi mbalimbali za wawania ...

Read More »

‘Serikali imekurupuka, imeumbuka’

Serikali imeingia doa. Migomo wafanyabiashara na madereva wanaoendesha mabasi ya abiria, imetikisa nchi kiasi cha kufanya wadau kadhaa kueleza kuwa nchi imekosa sifa za uongozi. Tukio la kwanza, ambalo limekuwa likijirudia linahusu wafanyabiashara ambao mara kwa mara wamekuwa wakigoma kwa kufunga maduka kwa shinikizo la kuachiwa Mwenyekiti wao, Johnson Minja. Tukio la pili ni la madereva, ambao Ijumaa iliyopita walitekeleza ...

Read More »

Siri ya Ugaidi

Kitendo cha nchi za Afrika Mashariki na Kati kuandaa mafunzo ya kudhibiti ugaidi, kinaelezwa kuwatia hasira kundi la al-Shaabab hadi kuvamia na kuua watu zaidi ya 150 nchini Kenya.   Jumla ya askari 300 kutoka nchi za Burundi, Rwanda, Tanzania, Uganda wamehudhuria mafunzo hayo yaliyoendeshwa na makomandoo kutoka nchi za Uholanzi na Marekani.   Mafunzo hayo yalifanyika nchini Rwanda na ...

Read More »

Mahakama ya Kadhi yamgeuka Pinda

Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameliweka njiapanda Bunge la Jamhuri ya Muungano, baada ya kuwalazimisha wabunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitisha muswada wa Mahakama ya Kadhi. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Msekwa Machi 21, mwaka huu. Katika mkutano huo aliwataka wabunge hao kuhakikisha muswada huo wanaupitisha kwa nguvu. Baadhi ya wabunge waliozungumza na gazeti hili walieleza kukasirishwa na kitendo ...

Read More »

Lowassa: Ninayaweza yote katika yeye anitiaye nguvu

  Hakuna ubishi kwamba minong’ono juu ya matamanio ya Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, au kutajwa kuwania urais, imeshika kasi.  Lowassa, Mbunge wa Jimbo la Monduli (CCM), amekuwa akitajwa kuwa miongoni mwa wanasiasa wenye nguvu kubwa na matamanio ya kuiongoza nchi baada ya utawala wa Rais Jakaya Kikwete.  Kutokana na kutajwa huko kwa Lowassa mara kwa mara, amekwepa kutangaza hadharani ...

Read More »

Jukumu letu ni kuboresha TPDC – Mwanda

  Kutokujiamini na kushindwa kuziendesha taasisi za umma nchini kwenda sawa na wakati, kumechangia kwa kiasi kikubwa mashirika mengi kufa na kuporomoka kiuchumi. Watafiti  wa masuala ya kiuchumi wanasema kujiamini na ubunifu ni nyenzo muhimu kwa pande mbili kati ya viongozi wenye nia thabiti na uzalendo unaolenga maslahi ya nchi na wananchi wote, bila kuwabagua katika makundi kati ya wachache ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons