Siasa

Haki ya Mtanzania inapogeuzwa anasa

Katika kipindi cha miaka kadhaa sasa, Watanzania wengi wanaishi kwa manung’uniko yanayotokana na kukosa haki zao za msingi huku waliopatiwa jukumu hilo wakiwabeza. Tumeshuhudia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) iliporatibu upatikanaji wa vitambulisho hivyo, huku wananchi wengi wakishindwa kuvipata.  Hakuna ubishi kwamba vitambulisho hivyo viliibua vurugu na hata kuhatarisha amani kwa baadhi ya maeneo. Ilikuwa ni mshikemshike. Shukrani kwa ...

Read More »

Vyombo vya habari ni UKAWA?

Mwanzoni mwa wiki iliyopita nilikuwa miongoni mwa watu waliojitokeza kuitumia haki yao ya msingi ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kwa mfumo wa kielektroniki (BVR), lakini kutokana na vituko vinavyoendelea haikuwezekana kuandikishwa. Kituo nilichokuwa nimepewa namba ya kuandikishwa kipo jirani kabisa na ninapoishi, ni ofisi ya serikali ya mtaa wa Mivumoni, Tegeta – Wazo jijini Dar es Salaam. ...

Read More »

Nani asiyependa kumeguka CCM inayobaka demokrasia?

Historia inaonesha kuwa vipindi fulani katika mustakabali wa nchi unalazimisha kupima nini ni janga zaidi ya jingine. Marehemu Samora Machel na Frelimo walikubali kutia saini Mkataba wa Nkomati wa ushirikiano na makaburu kama mkakati wa kujinusuru, na kutoa nafasi kukabili janga kubwa kuliko yote wakati huo, la kuondolewa Serikali ya Frelimo na Renamo ikisaidiwa na makaburu. Wakomunisti wa Afrika Kusini ...

Read More »

Lowassa kuhamia Chadema hajabadili uraia

Edward Ngoyai Lowassa kaamua kufanya mabadiliko ya kweli ya siasa hapa nchini. Kakihama chama chake cha siku zote na kuingia kwenye chama kingine, chama kikuu cha upinzani hapa nchini – Chadema. Huo ni uamuzi ambao Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, kaamua kuupa jina la kubadilisha gia hangani. Tukio hilo limetazamwa kwa hisia mbalimbali zilizo tofauti na wananchi. Wapo waliolipenda na ...

Read More »

Yah: Eti ngoma ya kitoto haikeshi? Nitathibitisha

Ngoma inogile – wale wa kucheza wanacheza na wale wa kushangilia wanashangilia na sisi watazamaji tunaoona utamu wa ngoma tumekaa pembeni kushuhudia mirindimo ya ngoma na mashairi yaliyopangika, ni burudani sana lakini ngoma yaelekea haitakesha mwisho ni alfajiri ya Oktoba. Sasa nchi yetu imeingia katika siasa ngumu ya kunadi kichama, kunadi sera zinazowezekana na zisizowezekana. Watanzania wengi wamekuwa ama wanachama ...

Read More »

Kweli tunahitaji mabadiliko?

Kwanza nianze kwa kuweka usahihi kwenye kichwa cha habari cha makala iliyopita katika safu hii ya Fasihi Fasaha.  Nilizungumzia juu ya “Usibadili bura yako na rehani”. Bura na rehani ni majina ya vitambaa vya hariri vyenye asili moja ya malighafi hariri ambayo ni nyuzi zinazotokana na viwavi vya mdudu nondo.  Vitambaa au nguo za hariri zina thamani na ubora mmoja. ...

Read More »

Tatizo siyo Edward Lowassa, ni Chadema

 Kupokelewa kwa Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kama mwanachama wa Chadema na kuteuliwa kwake kuwa mgombea urais wake ndani ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kunapaswa kuwaacha hoi Watanzania wengi. Hoi kwa maana ya kushuhudia namna ambavyo chama cha siasa kilichojipambanua kuwa mstari wa mbele kupinga watu na mifumo inayokiuka misingi ya ...

Read More »

Tumekosea barabara za mwendo kasi (1)

Nianze hoja yangu kwa kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uhai na amani ndani ya mioyo yetu, na hatimaye kuweza kuyafanya mengi tuyafanyayo kila kukicha likiwamo hili la ujenzi wa barabara za kuwezesha mabasi kwenda mwendo kasi. Kwa mantiki hiyo ni vema na haki na kila wakati kumshukuru Mwenyezi Mungu aliye mwingi wa rehema na mwenye kutujali muda wote wa ...

Read More »

Makongoro Nyerere: Nichagueni ninyooshe nchi

Mwaka huu ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu. Ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) tayari wamejitokeza watangaza nia 40 ambao wote wanawania kiti cha urais, waweze kumrithi Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu. Kila anayetangaza nia anayo maono ya nini anataka kuifanyia nchi hii kwa nia njema ya kututoa hapa tulipo tusonge mbele zaidi. Katika makala ...

Read More »

Wachina wabuni uhujumu uchumi mwingine

Kwa sasa kumetokea mchezo mchafu unaofanywa na raia wa China na Singapore walio hapa nchini. Mchezo huu umeshamiri baada ya baadhi ya Wachina wasio waaminifu kushiriki biashara ya pembe za ndovu. Wameanzisha utaratibu wa kusajili kampuni za kusafirisha samaki hai aina ya kaa na kamba kochi kwenda nje kwa kutumia kampuni zenye majina ya wazawa. Wanachofanya ni kutafuta Mtanzania, wanampa ...

Read More »

Namhurumia Rais ajaye

Wakati mwingine Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete mwenyewe anatuanzishia mada zinazotufanya tumjadili. Hatupendi kumwandama Rais wetu, lakini kauli zake zinatufanya tujitose kumkosoa kwa sababu ya kuweka rekodi sawa sawa. Wiki iliyopita alinukuliwa akitetea uamuzi wa Serikali yake, ambao kimsingi ni uamuzi wake, wa kulifanya deni la Taifa sasa kugota Sh trilioni 40. Mwezi Juni, mwaka huu, Waziri wa Fedha aliliambia Bunge ...

Read More »

Yah: Hali ya kila anayedhani anaweza kuwa kiongozi

Kama kuna kitu kinanikera ni hii tabia ya mtu kukurupuka kutoka nyumbani kwake na kuita watu wachache wanaomjua na aliowanunua wa mtaani kwake, na kutangaza nia ya kuomba ridhaa ya wananchi kuwa kiongozi wao. Kuna watu nadhani huwa hawajiangalii hata katika kioo achilia mbali kuuliza watu wenye akili kama wanatosha wanachotaka kufanya, au wataonekana vioja kwa hicho cha kutaka kutangaza nia ...

Read More »

Nani kasema wanawake hawawezi?

Vyama vya siasa vilivyowahi kuanzishwa kati ya mwaka 1927 na 2015 katika nchi ya Tanganyika, Zanzibar hata Tanzania havikubahatika kubuniwa, kuasisiwa wala kuongozwa na wanawake bali ni wanaume tu. Huu ni msiba mkubwa kwa akinamama, lau kama zipo sababu za utetezi. Hata kama wanawake hawakujimudu kubuni, au kuasisi vyama vya siasa, ukweli waliweza kushawishi, kuhamasisha na kuvuta wake kwa waume ...

Read More »

Changamoto za kulea watoto Tanzania

Utafiti uliofanyika nchini Uingereza unaonyesha kuwa gharama kwa wazazi ya kutunza mtoto kuanzia anapozaliwa mpaka kutimiza miaka 21 zilikuwa ni Paundi (£) 227,267 za Uingereza. Hii ni taarifa ya mwaka 2014 na ni kwa mujibu wa kituo cha utafiti wa uchumi na biashara kinachojulikana kwa Kiingereza kama Centre of Economic and Business Research (CEBC). Si gharama ndogo hata kwa Waingereza ...

Read More »

Jihadhari; haya ni mazingira ya kufutiwa umiliki wa ardhi

Watu wengi wana maeneo lakini wameyatelekeza. Kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi, Sura ya 113, kutelekeza eneo ni kosa ambalo mtendaji wake ambaye ni mwenye eneo anatakiwa kuadhibiwa. Nitoe tahadhari kuwa si vema watu kujisahau baada ya kuwa wamemiliki maeneo. Wakati mwingine si rahisi kujua kama suala la kufutiwa umiliki lipo kama halijakufika. Lakini, amini lipo, na wapo watu wamefutiwa umiliki ...

Read More »

Wale wa Lowassa, msiwe kama Petro

Kwanini awe ni Lowassa na si wengine waliotia nia ya kuwania urais? Ukimshtukiza mtu yeyote na kumuuliza ni kada gani kati ya hao waliotia nia angependa awe rais ajaye, kila mmoja atatoa jibu lake kutokana na mapenzi aliyonayo kwa mgombea wake. Na mimi napenda kutumia makala hii kutoa sababu zinazonifanya nimkubali Edward Lowassa. Awali ya yote natanguliza kuwaomba radhi Watanzania ...

Read More »

Kiburi chanzo cha ajali

Ajali ya gari iliyoua watu 23 papo hapo na kujeruhi wengine 34, imeongeza maumivu mengine kwa Watanzania ambako sasa takwimu zinaonesha zaidi ya abiria 1,000 wamepoteza maisha. Ajali iliyotokea usiku wa kuamkia Jumatatu iliyopita ilihusisha basi la Kampuni ya Another G kugongana na lori eneo la Kinyanambo A, Mafinga wilayani Mufindi, ikiwa ni takribani miezi mitatu baada ya ajali nyingine ...

Read More »

Kampuni yatelekeza minara ya simu

Minara 292 ya mawasiliano iliyojengwa na Kampuni ya Simu ya Excellentcom Tanzania mwaka 2008, imetelekezwa bila kutoa huduma yoyote, JAMHURI linaripoti. Baada ya kuitelekeza kwenye viwanja ambavyo baadhi vina makazi ya wamiliki wa ardhi hiyo, kumefanya kampuni hiyo sasa kudaiwa mamilioni ya shilingi ya kodi za pango la eneo. Kampuni ya Excellentcom Tanzania Limited ilisajiliwa kwa Wakala wa Usajili wa ...

Read More »

Ngeleja anaamini katika haya

Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja, ameahidi wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwamba endapo atafanikiwa kuteuliwa na chama chake na baadaye kuchaguliwa na Watanzania, kazi itakayokuwa mbele yake ni kuhakikisha uchumi wa Mtanzania mmoja mmoja unakua. Katika mahojiano kati yake na mwandishi wa makala hii yaliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Ngeleja anasema; “Hicho ndicho ninachokiamini ili kuleta maana ...

Read More »

Vijana wapewe nafasi Uchaguzi Mkuu (2)

Taifa linatarajia mabadiliko makubwa katika uchaguzi wa mwaka huu! Gazeti la Mwananchi Toleo No. 5419 la Jumatano Mei 27, 2015 uk. 33 limeelezea hoja zinazojitokeza kuhusu umri wa wagombea.  “HOJA ZA UJANA, UZEE katika vuta nikuvute uongozi wa Tanzania” habari kamili iliandikwa katika uk.  wa 36. Hapa ingefaa tuone busara za uongozi uliopita ulitathmini namna gani uzee na ujana wa ...

Read More »

Shwekelela: Nikiwa mbunge Kyerwa itaendelea

Homa ya uchaguzi imeikumba wilaya mpya ya Kyerwa, ambapo sasa Pancrace Shwekelela anasema “wakati ukifika nitatangaza nia ya kugombea ubunge katika Jimbo la Kyerwa baada ya kushawishiwa na watu, vikundi na marafiki zangu.” Jimbo la Kyerwa kwa sasa linashikiliwa na Eustace Katagira (CCM). Amekuwa mbunge wa Kyerwa kwa miaka 10. Katagira alilikomboa Jimbo hili kutoka kwa mbunge wa Upinzani, Benedicto ...

Read More »

CCM ‘wasipogawana mbao’ nitashangaa!

Kiongozi wetu Mkuu anaendelea na ziara ya kuwaaga marafiki wetu wa maendeleo. Anazidi kuongeza idadi ya safari na siku alizokaa ughaibuni. Kwa Afrika, amejitahidi kuwaga kwa pamoja pale nchini Afrika Kusini. Lakini kwa Ulaya, Asia na Marekani, naona kaamua kwenda kuaga kila nchi kadri anavyoweza. Hii haishangazi kwa sababu kwa miaka 10 safari zake nyingi zimekuwa za Ulaya, Marekani na ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons