Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana ametembelea shamba la mbegu la Global Agency Farm lililopo Buchurago Bugorora wilayani Misenyi Mkoa wa Kagera.

Akiwa shambani hapo, Kanali Mstaafu Kinana alishuhudia shughuli mbalimbali zinazofanyika katika uandaaji wa mbegu bora za mahindi ukiwa utekelezaji wa Ilani ya Uchagu ya CCM.

Pichani Kinana akiwa na viongozi wengine akiwemo Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila wakiwa wamepanda kwenye
mtambo unaotumika kwa shughuli za kilimo katika shamba hilo.

Kinana ambaye ameongozana na Shaka amehitimisha ziara yake mkoani Kagera na kuelekea mkoani Geita kendelea na ziara hiyo yenye lengo la kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025.

By Jamhuri