Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Matawi ya Yanga Dar es Salaam, Boas Ikupilika, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji amewaahidi kuisuka Yanga mpya kwenye dirisha dogo la Novemba.

Manji pia ameahidi kumpa sapoti kubwa Kocha Mwinyi Za­hera kuhakikisha sifa ya Yanga inarejea kwani amewakubali wachezaji baada ya kuwaona kwenye Uwanja wa Taifa hivi ka­ribuni alipokwenda kuwaangalia.

Usajili wa dirisha dogo umepangwa kuanzia Novemba 15 hadi Desemba 15, mwaka huu ambapo timu hupata nafasi ya kuongeza wachezaji wach­ache kulingana na upungufu wao.

Ikupilika amethibitisha kuwa Manji amekuwa akihusika katika mambo mbalimbali ndani ya klabu, amemuahidi Zahera kuwa, atamsaidia kutimiza ma­hitaji yake kwa kufanya usajili wa wachezaji ambao atahitaji kwenye dirisha dogo.

“Manji aliomba muda kidogo kabla ya kurejea rasmi wakati wowote, lakini kuna baadhi ya majukumu ambayo amekuwa ak­itekeleza kama kiongozi wetu. Amekuwa akishauri mambo mengi kuhusu timu yetu,” alidokeza kion­gozi huyo na kuongeza:

“Kikubwa baada ya kuiona timu, aliiamini na kututaka na wengine tuiamini kwa sasa lakini kwenye kipindi cha dirisha dogo yeye atafanya usajili, lakini kwa sasa kwa kuwa dirisha limefungwa tuwaamini waliopo na tuisaidie timu.

“Pia alizungumza na kocha na alikubaliana naye kwamba atampa mahitaji yake kwenye usajili wa dirisha dogo,” alisema katibu huyo ambaye huingia kwenye vikao vikubwa vya klabu.

1578 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!