Ndugu Mhariri

Natamani Watanzania kwa ujumla wetu tuwe na uelewa wa nguvu wa vyombo vya habari. Ikiwezekana tuingie barabarani kuishinikiza serikali iondoe sheria nzima ambayo ni kandamizi dhidi ya vyombo vya habari hivi.

Labda niwaombe jambo moja, vipi kama mkiipinga serikali kutochimba madini ya uranium kwa kuzingatia madhara ya kiafya yatokanayo na uchimbaji?

Kwa ka-data kadogo nilikonako ni kwamba Mataifa Makubwa yenye kuumia nishati imewawia ngumu kudhibiti athari za madini haya.

 

Majuzi tulishuhudia vinu vya Japan vilivyokuwa nje ya uwezo wao kwa dhibiti.

Tukumbuke jambo moja wanataka mali tu ili wenye mali ambao ni Mtanzania hazingatiwi wana mazingira wako wapi?

Nadhani una uwezo zaidi yangu ya kutafuta data kwenye vyanzo vingine kama Google na tuianike madhara ya madini haya.

Mtazamo wangu kama serikali yetu inatumia asilia zetu kirafi wakati nje zingine zinategemea bandari tu, tuwajibu tuwajibike Watanzania.


1249 Total Views 3 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!