Hivi karibuni taasisi ya Oakland imetoa taarifa yenye kichwa
cha habari: “Loosing the Serengeti: The Maasai land
that was to run forever”, na kutangazwa na mashirika
kadhaa ya habari ya kimataifa duniani kote.
Serikari ya Tanzania imeshutumiwa kwa uongo kwamba
inakandamiza haki za Wamaasai wanaoishi Wilaya ya
Ngorongoro inayopakana na Hifadhi ya Taifa Serengeti.
Taarifa hiyo inakwenda mbali zaidi na kudai kwamba
Tanzania imekuwa ikitumia sababu za kiikolojia ili kuwapa
nafasi wawekezaji waliopo eneo hilo kwa kuangalia zaidi
maslahi ya kifedha kupitia utalii.

2

Taarifa hiyo ni mwendelezo wa kampeni ambazo zimekuwa
zikifanywa na taasisi zisizo za kiserikali (NGOs) zinazofanya
kazi la Loliondo ambazo zimekuwa zikisambaza taarifa za
uongo na uchochezi. Taarifa hizo potofu zimekuwa zikiibua
hisia kali miongoni mwa jamii dhidi ya Serikali kwa malengo
ya kukusanya fedha kutoka kwa wafadhili waliopo ndani na
nchi za nje.
Baada ya Kamati Shirikishi ya kutatua mgogoro wa
ardhi katika Pori Tengefu Loliondo iliyoundwa na
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kuwasilisha taarifa
yake Aprili, 2017, Waziri Mkuu alisema kwamba sasa
mwanga wa kutatua mgogoro wa Loliondo
umeonekana. Na baadaye Waziri Mkuu alitoa
maelekezo ya Serikali baada ya kuzingatia maslahi
mapana ya taifa na jamii, na kuwa na maelekezo hayo
yatamaliza kabisa mgogoro huo uliodumu kwa
takribani miaka 26. Katika maelekezo yake (tamko
hilo,) Waziri Mkuu alisema Serikali imezingatia
maslahi ya pande zote na hivyo kutaundwa chombo
maalum cha kusimamia eneo hilo.
Tamko hilo halikuwapendeza baadhi ya wenye NGOs
wanaotumia migogoro ya ardhi Loliondo kama sehemu ya
kuendesha maisha yao ya kila siku.
Maandalizi ya mikakati mipya yakaanza ambako Alais Melau
wa PWC na Sinandei Makko wa UCRT walikwenda

3

Marekani kuonana na taasisi mbalimbali ikiwamo Oakland
Institute ili waibue hoja hiyo ya mgogoro wa Loliondo
kutokea nje ya nchi, kwani Maanda Ngoitiko alikuwa na
uhusiano wa karibu na Anuradha Mittal ambaye ni
mwanzilishi wa Oakland Institute.

JINSI OAKLAND INSTITUTE WALIVYOKUWA
WANAKUSANYA TAARIFA

Kati ya mwaka 2011 na 2013 Oakland Institute waliendesha
kampeni kupinga mradi wa kilimo uliokuwa ufanyike katika
eneo la Katumba na Mishamo nchini Tanzania, chini ya
mpango wa Kilimo Kwanza ambao ungeendeshwa na
kampuni ya AGRISOL ya Marekani. Anuradha Mittal
alikuja nchini kipindi hicho alianza kuwa na uhusiano na
baadhi ya NGOs nchini zilizokuwa zikijishughulisha na
masuala ya migorogo ya ardhi.
Mwaka 2015, Mittal aliombwa kwenda Loliondo na
Mkurugenzi wa PWC Maanda Ngoitiko kufuatilia mgogoro
wa ardhi kati ya Kampuni ya Thompson Safaris Ltd na Kijiji
cha Sukeinya (baadaye kwa maneno yake Mittal akimwambia
mwakilishi wa kampuni ya Thompson walipokutana nchini
Marekani alisema, “Nilimwambia Maanda kwamba mimi nilipewa
P.I miaka ya nyuma nchini Tanzania, hivyo itakuwa vigumu mimi
kuja huko. Hivyo mpango wa mimi kuja huko uliandaliwa kupitia

4

nchini Kenya ambako nilichukuliwa kwa pikipiki kutoka mpaka wa
Posmolu hadi kijijini ambako nilikuta gari na wenyeji wangu
wananisubiri…”)
Mwaka 2017 Oakland Institute walitakiwa waanze
kukusanya taarifa ambazo zingetumika kuandaa ripoti
kinzani dhidi ya mgogoro wa Loliondo na mpango mzima
wa Serikali ambao ulikuwa unaonyesha kwamba wawekezaji
waliopo katika eneo hilo wataendelea kuwepo huku shughuli
za kiuhifadhi na za kijamii zikiendelea pia kufanyika kwa
utaratibu maalumu.
Kwa kuwa Anuradha Mittal wa Oakland Institute
alishasema kwamba haruhusiwi kuingia Tanzania, hakuwa
na njia nyingine ya kupata taarifa zaidi ya kuwatumia
mawakala ambao aliwapa jina la “Ground Researchers”.

MALIASILI INITIATIVES
Agosti 2017, Fred Nelson mwanzilishi wa taasisi ya Maliasili
Initiatives iliyopo Olasiti, Arusha alipewa kazi na Oakland
Institute kama wakala wa kukusanya taarifa walizokuwa
wanazihitaji kuhusu mgogoro wa Loliondo ambazo
zingetumika kuandaa ripoti yao.

5

Fred Nelson
Nelson awali alikuwa anafanya kazi na taasisi ya Tanzania
Natural Resource Forum ( TNRF), lakini baadaye aliondoka
na kurudi Marekani, kwa uzoefu wake nchini Tanzania
alionekana atafaa kwa kazi hiyo. Hivyo, basi ilibidi aje na
familia yake (mke na watoto wawili) kwani hiyo kazi
ingechukua muda.
Kwa kupitia taasisi ya Maliasili Initiative ilikuwa ni rahisi
kwa Nelson kukusanya taarifa kutoka taasisi pacha za PWC
na Ujamaa Community Resource Team (UCRT) ambao
viongozi wake ni Maanda na Makko ambao ni mke na
mume.
Kwenye kazi hiyo, Nelson ameshirikiana na:

Jessie Davie

6

1: Jessie Davie kutoka California Marekani, Ni mfanyakazi
wa taasisi ya Maliasili Initiative, ambaye aliwahi kufanya kazi
TNRF na kwa nyakati tofauti amekuwa akifanya kazi na
PWC ikiwa pamoja na hivi karibuni kutengeneza
mapendekezo ya jinsi ya kuendesha shughuli za utalii
kwenye eneo la Loliondo ambalo NGOs kadhaa zimetaka
liitwe LAMA.
Jessie anaishi nchini akiwa na mume wake Jessy anayefanya
kazi UN-MICT Arusha (haijulikana kama viza ya Jessie ya
kuingia nchini ni ya kifamilia au ni ya kikazi).

Cara Scott
2: Cara Scott, huyu ni raia wa Uingereza. Kama alivyo Jessie,
ni mfanyakazi wa Maliasili Initiatives. Kwa nyakati tofauti
amekuwa akifanya kazi na PWC na UCRT akiwa ni
kiunganishi cha taasisi hizo na wafadhili waliopo nje ya nchi.

7

Ni mke wa Wakili Rashid Rashid wa kampuni ya KNR
Legal iliyopo Arusha ambaye pia ni wakili ambaye
anaiwakilisha jamii ya vijiji vya Mondorosi, Soitsambu na
Sukenya kwenye kesi iliyopo Mahakama ya Rufaa dhidi ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kampuni ya
Thomson. Ni wakili wa Maanda Ngoitiko dhidi ya Diwani
wa Oloipiri, William Alais na Padri Gabriel Killel. Rashid
akishirikiana na Lauren Carasik wa Western New England
University waliiwezesha taasisi ya Earth Rights International
ya Marekani kuwasaidia wafnavijiji wa Mondorosi,
Soitsambu na Sukenya kufungua kesi maarufu kama
“STOP THOMPSON” nchini humo, ambako mahakama
iliiamuru kampuni ya hiyo kutoa nyaraka zinazoihusu
(Discovery order). Nyaraka hizo zimetumiwa na Oakland
Institute kama taarifa za rejea kwenye ripoti yao.
Siku mbili kabla ya ripoti ya Oakland kutolewa, Nelson na
Jessie waliondoka nchini na kwenda Kenya ambako
inasadikika kwamba wanataka kuhamishia ofisi yao huko
kabla ya Juni, mwaka huu.

SUSANNA NORDLUND
Oakland Institute wamemtumia pia Susanna Nordulund
ambaye ni raia wa Sweden ambaye ana ushirika wa karibu
mno na Maanda Ngoitiko wa PWC na baadhi ya wanasiasa
wa Wilaya ya Ngorongoro kuanzia ngazi ya vijiji hadi wilaya.

8

Kwa mara ya kwanza aliingia Ngorongoro akiwa ni
‘volunteer’ kwenye taasisi ya PWC. Baadaye aliendelea kuja
nchini na ikabainika kwamba alikuwa akiendesha mikutano
na wananchi na NGOs zenye malengo ya uchochezi.
Serikali ilimfukuza nchini kwa PI. Pamoja na kunyimwa
ruhusu ya kuingia nchini, kwa msaada NGOs aliweza
kuingia kwa kupitia Kenya kisha akaingia Ngorongoro kwa
njia za panya.
Susanna aliendelea kuishambulia Serikali ya Tanzania kupitia
mitandao ya kijamii akisaidiwa kupata habari na nyaraka
mbalimbali kupitia kwa mamluki wake waliopo nchini. Hapa
miongoni mwa wanaotajwa-tajwa ni Maanda Ngoitiko,
Samwel Naingiria, na mmoja wa mawaziri katika Baraza la
Mawaziri la sasa.
Taarifa alizowapa Oakland Institute amezichapisha pia
kwenye blog yake ya “View from the Termite Mound”.
Hadi sasa anaendelea kuitetea ripoti hiyo kwenye mitandao
ya kijamii.

PASTORAL WOMEN COUNCIL (PWC)
Pastoral Women Council (PWC) chini ya Maanda Ngoitiko
ni NGO iliyoanzishwa mwaka 1997 ikiwa na ofisi zake
katika Kata ya Olasiti jijini Arusha na Loliondo wilayani
Ngorongoro. Shirika hili limekuwa likiendesha shughuli
zake katika Wilaya ya Ngorongoro tangu lilipoanzishwa hadi

9

kufikia mwaka 2009 ambako ilitanua wigo na kuingia hadi
Wilaya ya Longido (kwa mujibu wa taarifa ya kazi ya mwaka
2012).
Tofauti na inavyofikiriwa, kazi asasi hii imekuwa na sura ya
kichochezi na kuendeleza migogoro katika Wilaya ya
Ngorongoro. Mwanzo taasisi hii ilijiweka karibu na jamii na
kuiaminisha kwamba ipo kwa ajili ya kutatua kero zao kwa
kutumia jitihada zao na pia michango ya wahisani.
Nadharia hii ilisababisha wadau, hasa wa nje ya nchi kuamini
yale yanayosemwa na asasi hii na kuzipa taarifa zao uzito
zikiamini ni sauti halisi ya jamii husika kufuatana na jinsi
jamii husika inavyoendeshwa na wanajamii wenyewe. Badala
yake imekuwa ikifanya kazi zinazoonekana kuwa ni zenye
manufaa zaidi kwa nchi jirani na kwa maslahi ya baadhi ya
kampuni za kitalii zilizoko hapa nchini.
Asasi hii imekuwa ikiwatumia akina mama waungwana wa
vijijini kwa ajili ya maslahi ya ‘wajanja wachache’ na
kutumika kwao ni kwa kuleta tawsira inayoonyesha kwamba
Serikali kwa ujumla wake haina uchungu kwa wananchi
wanaoishi Loliondo.
Suala la kuwahamisha Wamaasai wa Loliondo limekuwa ni
ajenda kubwa kwao kwani limeonekana lina mvuto kwa
wafadhili waliopo mataifa ya nje. Ndiyo maana imekuwa
rahisi kwa taasisi ya Oakland kubeba hiyo ajenda.

10

MIKAKATI ILIYOPO SASA HIVI
Mkakati uliopo ni kufanya kampeni za kudai haki za ardhi
na za jamii ya Kimaasai kwa kutumia vyombo vya habari
vikubwa vya ndani na nje ya nchi.
Hivi karibuni PWC wakishirikiana na taasisi ya African
Initiatives waliandaa semina ya kujenga uwezo (capacity
building) kwa NGOs yaliyopo Arusha. Semina hiyo
ilifanyika katika hotel ya City Link. Mtoa mada alikuwa ni
mwakilishi wa taasisi ya HAKIELIMU. Washiriki
walifundishwa mbinu mbalimbali za kuishinikiza Serikali
kupitia vyombo vya habari. Mifano hai ilitolewa ni kwa jinsi
gani wawekezaji waliopo Loliondo wanaweza kuondolewa
ikianzishwa kampeni ya kuwachonganisha na Serikali ya
Tanzania kwa kutumia vyombo vya habari, hasa vya nje.
Mwakilishi wa PWC aliwaambia washiriki wa semina hiyo
kwamba fedha za kufanya kampeni hiyo zitapatikana kutoka
kwa taasisi za African Initiatives na Maliasili Initiatives.
Ahadi na kazi hiyo vimeanza kuonekana kwa Tanzania
kuchafuliwa kwenye vyombo vya habari karibu duniani kote.
Hii ndiyo hatari inayotokana na Serikali kuwa na kigugumizi
katika kumaliza mgogoro wa Loliondo.

3433 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!